Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan alihudhuria kongamano la kimataifa lenye mada "Watoto na Vijana Kazini/Mabadiliko ya Hali ya Hewa katika Asia ya Kati" kama sehemu ya Siku ya Watoto Duniani. / Picha: AA

Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan, ambaye yuko pamoja na Rais Recep Tayyip Erdogan katika ziara yake katika mji mkuu wa Uzbekistan Tashkent kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi, amekutana na wenzi wa viongozi waliokuja nchini humo kwa ajili ya kikao.

Katika ziara yake, Erdogan alihudhuria kongamano la kimataifa lililokuwa na mada ya “Watoto na Vijana Kazini/Mabadiliko ya Tabia nchi katika Asia ya Kati” lililofanyika kama sehemu ya Siku ya Watoto Duniani, ambayo itaadhimishwa tarehe 20 Novemba.

Katika kongamano hilo, maafisa kutoka Umoja wa Mataifa na nchi mbalimbali walijadili kukuza elimu ya mazingira na umuhimu wa jukumu la watoto na vijana katika kukabiliana na janga la hali ya hewa.

"Nilielezea jitihada za mazingira na hali ya hewa zilizofanywa Uturuki kwa watoto na vijana, ambao ni walengwa muhimu zaidi na pia wahusika wakuu wa Mpango wa Zero Waste ambao tulianza miaka sita iliyopita," alisema Erdogan.

"Katika hafla ya mpango huu wa maana ambapo mustakabali wa watoto unajadiliwa, nilielezea tena hali ya uchungu ambapo watoto wa Kipalestina wanachukuliwa maisha yao bila huruma," aliongeza, akimaanisha mzozo wa Israeli na Palestina tangu Oktoba 7 ambapo hadi sasa zaidi ya watoto 4,400 huko Gaza wameuawa katika mashambulizi ya Israel.

Vita vya kikatili vya Israel dhidi ya Gaza

Jeshi la Israel limeendelea na mashambulizi yake ya anga na ardhini huko Gaza, ambayo imekuwa chini ya mashambulizi ya anga tangu shambulio la kuvuka mpaka la Hamas tarehe 7 Oktoba.

Licha ya idadi ya kushangaza ya Wapalestina 10,000 waliouawa tangu siku hiyo, kulingana na Wizara ya Afya katika eneo hilo, idadi hiyo huenda ikawa "juu kuliko inavyotajwa," mwanadiplomasia mkuu wa Marekani alisema.

Israel imekubali kuanza kila siku "kusimama kwa kijeshi" kwa saa nne kaskazini mwa Gaza ili kuruhusu watu katika eneo hilo kukimbia vita, White House ilisema leo.

TRT World