Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa wito kuhusu jukumu linalozidi kuongezeka la migogoro ya maji katika kuchochea mizozo duniani kote.
“Migogoro mingi katika Asia, Amerika, Afrika Kaskazini, na Mashariki ya Kati inatokana na mizozo juu ya vyanzo vya maji,” Erdogan alisema Ijumaa katika hotuba yake kwenye mkutano kuhusu kilimo ulioandaliwa na benki ya serikali ya Uturuki, Ziraat Bank huko Istanbul.
"Kutokana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi, vyanzo vya maji na mabwawa vinakuwa maeneo ya mizozo," aliongeza. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa wito kuhusu jukumu linalozidi kuongezeka la migogoro ya maji katika kuchochea mizozo duniani kote.
Kuzuia njaa
Erdogan pia aligusia makubaliano ya nafaka ya Bahari Nyeusi ambayo Uturuki na Umoja wa Mataifa walipatanisha kati ya Urusi na Ukraine mnamo 2022.
"Kama sio kwa ajili ya makubaliano ya nafaka ya Bahari Nyeusi, yaliyoongozwa na Uturuki, maeneo mengi yangeteseka kutokana na njaa, hasa nchi za Afrika," alisema.
Rais alisisitiza kuwa Uturuki "ilizuia hali kuwa mbaya zaidi kwa kuhakikisha kupitishwa kwa tani milioni 33 za nafaka kupitia milango yetu ya bahari" wakati wa janga la Uviko-19 na vita vya Ukraine.