Mke wa rais wa Uturuki Emine Erdogan anapanga kutoa msaada kwa watoto wa Palestina wanaohitaji msaada na utunzaji, Mahinur Ozdemir Goktas Waziri wa Huduma Jamii na familia wa Uturuki amesema.
Waziri Mahinur alisema kwenye mtandao wa X kwamba alizungumza na Waziri wa Masuala ya Wanawake wa Palestina Amal Hamad na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Ahmed Majdalani kuhusu mpango huo katika mkutano uliofanyika kupitia mtandao siku ya Jumapili.
"Kwenye mazungumzo yetu, nilieleza wasiwasi wetu wa dhati na huzuni juu ya shida za kibinadamu na mashambulio mabaya kwa raia huko Gaza," alisema.
"Nilisisitiza kujitolea kwetu kuendelea na mshikamano wenye misingi na maadili ya kibinadamu na watu wa Palestina mbali na kila aina ya siasa kupitia ushirikiano kati ya wizara zetu," alisisitiza Goktas.
Goktas aliongeza kuwa alitoa pendekezo la mpango wa pamoja, chini ya uongozi wa Mama Emine Erdogan, kutoa "msaada wa haraka kwa watoto" walioathiriwa na uvamizi wa hivi karibuni wa Israeli.
"Nia yetu ni kutoa matibabu, ulinzi na utunzaji kwa wale watoto ambao wamejeruhiwa au kuchwa yatima kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na Israeli, hadi uhasama kama huo utakapokoma," alisisitiza.
Kama sehemu ya juhudi hizi, walikubaliana kuanzisha vikundi vya pamoja vya kazi, "kuzingatia majukumu ya wizara zote mbili na wenzao wa Palestina," alibainisha Goktas.
Msimamo dhabiti wa uturuki
"Nataka kusisitiza dhamira yetu imara ya kuchukua kila hatua inayowezekana ndani ya mfumo wa sheria ya kimataifa kumaliza mashambulizi na uvamizi unaoendelea, kuhakikisha kuwa Wapalestina wanaweza kufurahia maisha ya uhuru na usalama katika nchi yao mapema," Goktas alisema.