Erdogan alisema "majaribio ya Israel ya kupindisha ajenda, kuficha ukatili huko Gaza pamoja na kuondoa hilo kwenye ajenda haipaswi kuruhusiwa kutokea." / Picha: AA  

Rais wa Uturuki amezitaka nchi za Magharibi kujibu kwa pamoja juu ya hatua za Israel huko Gaza, kama zilivyoitikia mashambulizi ya hivi majuzi ya kulipiza kisasi ya Iran.

"Tumeona nchi za Magharibi zikijibu kwa kauli moja kulipiza kisasi dhidi ya Iran. Wahusika hawa wanahitaji kuungana katika kuiambia Israel 'inatosha'," alisema Recep Tayyip Erdogan katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jijini Ankara, siku ya Alhamisi.

Iran ilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya Israel siku ya Jumamosi ili kulipiza kisasi shambulio la anga la Aprili 1 kwenye jumba lake la kidiplomasia katika mji mkuu wa Syria. Iran ilirusha zaidi ya ndege 300 zisizo na rubani na makombora, huku takriban zote zikinaswa na mifumo ya ulinzi ya anga ya Israel na washirika wake - Marekani, Ufaransa na Uingereza.

"Moja ya mauaji makubwa zaidi ya karne iliyopita yamekuwa yakitokea Gaza kwa siku 195. Ni lazima tuongeze juhudi kukomesha mauaji huko Gaza," rais wa Uturuki alisema. "Usitishaji mapigano wa mara moja na wa kudumu lazima ufikiwe haraka iwezekanavyo, na kisha lazima tuchukue hatua za kufikia suluhisho la serikali mbili."

Erdogan alisema "Israel inalenga kupindisha ajenda, kuficha unyama wake wa Gaza na vile vile kuondoa ajenda hii nzima, hili halitovumilika."

Israel imefanya mashambulizi makali ya kijeshi huko Gaza tangu Oktoba 7, 2023 mashambulizi ya kuvuka mpaka ya kundi la Palestina Hamas ambapo karibu watu 1,200 waliuawa.

Takriban Wapalestina 34,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameuawa tangu wakati huo, kando na kusababisha makazi yao, uharibifu na hali ya njaa.

TRT Afrika