Erdogan amefanya mazungumzo na Zelenskyy Istanbul / Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemueleza mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kuwa Kiev ilistahili kujiunga na NATO, lakini pia ameiambia ifanye mazungumzo ya amani na Moscow.

"Hakuna shaka kwamba Ukraine inastahili uanachama wa NATO," Erdogan aliambia mkutano wa pamoja wa vyombo vya habari na rais wa Ukraine mapema Jumamosi, akiongeza kuwa "pande zote zirejee kwenye mazungumzo ya amani".

"Kwenye vita ambavyo vinaingia siku ya 500, watu wa Ukraine wanatetea uadilifu wa mipaka yao na uhuru wa nchi yao. Tangu hatari ya migogoro ilipoibuka, tulifanya kila juhudi kuzuia vita," alisema Erdogan.

Uturuki imefanya "juhudi za juu zaidi kukomesha" vita vya Urusi na Ukraine kupitia mazungumzo "kwa misingi ya sheria za kimataifa," aliongeza.

"Ningependa kusisitiza tena jambo ambalo nimekuwa nikilitetea siku zote: Amani yenye haki haina mshindi wala aliyeshindwa. Licha ya tofauti za maelewano kati ya pande zote, ni nia yetu ya dhati kurejea usakaji amani haraka iwezekanavyo." Erdogan alisema.

Zelenskyy alizuru Uturuki Ijumaa kujadili uhusiano, masuala ya kikanda na kimataifa, pamoja na matukio ya hivi karibuni katika vita, mkataba wa nafaka wa Bahari Nyeusi na kuhakikisha amani na utulivu katika eneo la Bahari Nyeusi.

Ilikuwa ni ziara yake rasmi ya kwanza nchini Uturuki tangu kuanza kwa vita vya Urusi na Ukraine vilivyoanza Februari 2022.

Kiongozi wa Uturuki alisema kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin atazuru Uturuki mwezi Agosti.

"Mwezi ujao Putin atafanya ziara Uturuki," Erdogan alisema, akiongeza kwamba alijadili kubadilishana wafungwa na kiongozi huyo wa Urusi.

"Ningependa kusisitiza tena jambo ambalo nimekuwa nikilitetea siku zote kwa msisitizo: Amani yenye haki haina wapotezaji. Licha ya tofauti za maelewano kati ya pande zote, ni nia yetu ya dhati kurejea usakaji amani haraka iwezekanavyo." Erdogan alisema.

Erdogan

Mpango wa biashara ya nafaka

Kuhusu mkataba wa nafaka wa Bahari Nyeusi, Erdogan alisema kuwa Ankara inafanya juhudi za kuurefusha kwa kipindi kirefu zaidi baada ya muda wake kukaribia kumalizika Julai 17.

"Tunafanyia kazi ni kwa muda gani tunaweza kurefusha mkataba huo baada ya Julai 17. Matumaini yetu ni kwamba, itaongezwa angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu, sio kila baada ya miezi miwili. Tutafanya juhudi katika suala hili na kujaribu kuongeza muda wake hadi miaka miwili," Erdogan alisema.

Juni mwaka jana, Uturuki, Umoja wa Mataifa, Urusi na Ukraine zilisaini makubaliano mjini Istanbul ili kurejesha usafirishaji wa nafaka kutoka bandari tatu za Bahari Nyeusi ya Ukrain ambao ulisitishwa baada ya vita vya Urusi na Ukraine kuanza Februari 2022.

Kituo cha uratibu wa pamoja na maafisa kutoka nchi hizo tatu na Umoja wa Mataifa kilianzishwa Istanbul ili kusimamia usafirishaji huo.

Kulingana na maafisa wa Uturuki, zaidi ya tani milioni 33 za nafaka zimesafirishwa kwa watu wanaohitaji.

Maafisa wa Urusi wamedokeza kuwa Moscow inaweza kuzuia kurefushwa kwa mpango huo mwezi huu, wakilalamika kwamba sehemu za kuruhusu usafirishaji wa mizigo ya Urusi hazijatekelezwa.

Uturuki, inayosifika kimataifa kwa nafasi yake ya kipekee ya upatanishi kati ya Ukraine na Urusi, imesisitiza mara kuwa kwa mara Kiev na Moscow wamalize vita kupitia mazungumzo.

Uongozi wa Uturuki katika kutekeleza mpango wa amani

Zelenskyy alisema Kiev inataka kutekeleza mpango wa amani wa nchi yake na akaeleza kuwa Uturuki ipo tayari kuongoza katika suala hili.

Zelenskyy pia amemshukuru Erdogan kwa ukarimu wa taifa lake katika kuwapokea raia wa Ukraine nchini Uturuki.

"Niko hapa Istanbul kumshukuru kila mtu anayeitakia amani nchi yetu na watu wetu," alisema Zelenskyy.

Alieleza kuwa anashukuru kwa msaada wa Uturuki katika kulinda mipaka ya Ukraine.

TRT World