Deniz Sapmaz, 13, amekua mchezaji wa gofu mdogo zaidi wa Uturuki katika nafasi za Gofu za chipukizi Duniani kufuatia mafanikio yake katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Demiz akizungumza na shirika la Habari Anodolu alisema wazazi wake walikuwa wachezaji wa gofu pia waliohusishwa na Klabu ya Gofu ya Atasehir na alianza kwa kupendezwa na mchezo huo kutokana na muda aliokaa katika klabu hiyo.
"Idadi ya marafiki waliongezeka baada ya muda, nilikuwa nikiburudika nao. Kisha nikaanza kuichukulia gofu kwa uzito zaidi. Ila pia unahitaji kufanya kitu ambacho kinafurahisha. " alisema Demiz.
Kigezo muhimu zaidi kwa wale wanaotaka kuanza mchezo huu ni nguvu ya kiakili, kulingana na mwanariadha huyu mchanga.
"Gofu sio tu mchezo unaojumuisha talanta na kazi. Ni zaidi yake kwani ni mchezo wa kiakili. Ikiwa huna nguvu kiakili, alama zako zinaweza pungua hivi hivi," alisema.
Demiz anataka kushinda Kombe la Evian Juniors, mashindano ya vijana chini ya miaka 14. "Nataka kushiriki Kombe la Evian Juniors kwa sababu ni mwaka wangu wa mwisho nikiwa na umri wa miaka 13. Mpango wangu wa siku za hivi karibuni ni kucheza katika LPGA (Chama cha Gofu cha Wanawake)," alisema.
Alipoulizwa kama anataka kuwa nambari moja duniani, mchezaji huyo mchanga alijibu kwa matumaini mno.
"Ikiwa nitakuwa wa kwanza katika viwango vya ubora duniani, kila kitu kitakuwa kizuri lakini nadhani nina muda zaidi mbele yangu. Ninaweza kuwa siku moja."
Kwa sasa Deniz yuko nafasi ya 1802 duniani baada ya kushinda katika kundi la umri wake kwenye "U.S. Kids Antalya Turkish Open 2023" mwezi Januari na pia "Kombe la Kimataifa la "5 Stars International" katika kitengo cha vijana chini ya umri wa miaka 15 nchini Poland mwezi Februari.