Moshi watanda wakati wa mashambulizi ya Israeli kwenye kiji cha Khiam Kusini mwa Lebanon, mnamo Juni 8, 2024. /Picha: AFP

Na Farah-Silvana Kanaan

Kuna jambo la kuhuzunisha sana kuhusu kuona watu kwenye mitandao ya kijamii wakijadili kwa furaha kwamba vita vinayosababisha mauaji ya halaiki heunda vikaanza dhidi ya nchi yako.

Kana kwamba ni mechi ya kandanda, au kutokea kwa Gaza ya pili, maneno matatu yanayotumiwa kuelezea Lebanoni ambayo si mbali sana, iwapo watu wabaya watapata njia yao.

Hata hivyo, licha ya vitisho halisi, yanayoonekana sana, na uungwaji mkono rasmi wa bila masharti na Marekani, maisha yanaendelea.

Katika chapisho la hivi majuzi la Facebook ambalo lilisambaa mitandaoni, Mlebanon aliyeko ughaibuni anauliza, "Je, ni salama kutembelea Lebanon?"

Jibu lilikuwa la kuchekesha kama lilivyokuwa la kudharau (lakini ni kweli bila ubishi): "Kulingana na Twitter, hapana. Kulingana na Instagram - ndio."

Tayari vitani

Sehemu ya kutisha zaidi ya haya yote ni kwamba Israeli tayari inaendesha vita huko Lebanon. Msisitizo wa wengi nje, lakini haswa ndani ya Lebanon kwamba vita vinaweza kutokea msimu huu wa joto, wakati watu wa Kusini wameingiwa na hofu na mlio wa mara kwa mara wa ndege zisizo na rubani za Israeli, kuharibiwa kwa maeneo mengi ya ardhi na fosforasi nyeupe, na takriban watu 450 waliouawa tangu Oktoba 8, ni jambo la Ukatili.

Takriban Walebanon 100.000 wa Kusini wamelazimika kukimbia makazi yao na maisha yao yote katika sehemu ya kusini ya Lebanon. Hii ni, kwa kipimo chochote, hali ya vita.

Haijalishi ni watu wangapi wanaoendelea kupiga kelele kwamba tulijiletea wenyewe kwa kuunga mkono upinzani— je, hatupaswi kulinda ardhi yetu ambayo viongozi na raia wa Israeli wanadai kuwa ni yao kila siku?

Maafisa wanahudhuria mazishi ya Kamanda wa Kijeshi wa Hezbollah, Mohammed Naamey Nasser, katika kitongoji cha kusini mwa Lebanon, mnamo Julai 4, 2024. /Picha: AFP

Inaonekana kama Lebanon haiko vitani kamwe na Israeli. Jambo ambalo ni la kushangaza, kwa sababu serikali yetu hata haitambui rasmi uhalali wa Israeli.

Israeli tayari imeshambulia miji mikubwa kama Saida, Sour na Baalbek. Imemuua kiongozi wa Hamas huko Beirut. Wanapenda kuamini kwamba Dahiye, kitongoji kilichoharibiwa na Israeli mwaka 2006 kama adhabu kwa madai ya kuunga mkono Hezbollah, ni kana kwamba ni eneo fulani lililojitenga na Beirut. Sio hivyo.

Ni kitongoji kilichojengwa upya, karibu na ninapofanya kazi. Ambapo watu wengi ninaowafahamu wanaishi na familia zao, wana moja ya duka nzuri zaidi la vitabu huko Beirut, na pia wanauza "mkate wa burger" bora zaidi katika mji.

Makumi ya watoto walijeruhiwa katika shambulio dhidi ya basi la shule, wanawake vijana waliuawa huko Sour, wafanyikazi wa ulinzi wa raia na waandishi wa habari wamelengwa kimakusudi. Hii tayari ni vita. Vita vya kisaikolojia na kimwili.

Mgawanyiko mkubwa

Bila shaka, kupanuliwa zaidi kwa vita katika maeneo mengine ya nchi ni hali ambayo hakuna mtu anataka kuona kutokea.

Ingawa wengine (mimi mwenyewe nikiwemo) wamejiuliza kwa sauti kubwa miezi hii tisa iliyopita (na mnamo, 2021, na 2014, na 2006, na na na): "Labda vita vya pande zote ndio vinapaswa kutokea, ikiwa hiyo hatimaye itatokea, na kusababisha kuporomoka kabisa kwa nchi ya Israeli, na kuwa mwisho wa kuikalia kwa mabavu Palestina, na ukombozi wake," hata hivyo hakuna anayetaka vita. Hakuna anayetaka kuuawa wala kutazama wapendwa wake wakiuawa.

Hakuna anayetaka kuiona Lebanon ikiwa kifusi tena. Sio ndege wa finiksi, ni nchi iliyojaa wanadamu. Na historia ya zamani. Na watu kupoteza masiha yao itawaathiri watu wengine.

Ni hali ya kawaida ya binadamu kutaka kuishi bila uwoga, kuishi katika utulivu, na licha ya kile Wazayuni (na washirika wao wenye nguvu) wanajaribu sana kukufanya uamini: Waarabu ni binadamu pia. Sisi ni watoto halisi wa nuru, ambao hatutaki chochote zaidi ya kutoka chini ya kivuli cha uharibifu unaoendelea.

"Walebanon wanafikiri," "Walebanon wanataka" - wachambuzi, waandishi wa habari, na watu waoga kwenye mitandao ya kijamii wanapenda kubashiri juu ya utendaji wa ndani wa "akili ya Lebanon," lakini mtu yeyote ambaye anaijua nchi hii badala ya kuitumia vibaya ili kuendeleza kazi zao au kuiona kama aina fulani ya mahali pa kizushi, anajua kwamba hakuna kitu kama hicho.

Ni nchi ambayo imegawanyika kwa kina, kwa undani. Baadhi yetu hawawezi kufanya kazi kwa shida, tukijua ndugu na dada zetu wamechinjwa jirani, na wamesambaratishwa kwa huzuni, kwa sababu hatufanyi lolote kulizuia hilo.

Wengine hawakujali kile kinachotokea kwa Wapalestina na wangekaribisha kufanya mahusiano i ya kawaida na Israeli. - "Ingekuwa bora kwa uchumi wetu," mtu aliniambia hivyo mara moja. Nikabalisha mtazamo wangu kuelekea kwao sikuwatazama tena kwa njia ile ile.

Moto na moshi unatanda baada ya makombora kurushwa kutoka kusini mwa Lebanon kulenga maeneo ya kaskazini mwa Israel mnamo Julai 4, 2024. /Picha: AFP.

Kusubiri na kutazama

Wengi wanashukuru kwa uwezo wa Hezbollah wa kulinda sio tu Kusini bali Lebanon yote.

Wengine wanailaumu Hezbollah kwa kila jambo linaloenda vibaya katika nchi hii na wangependa kuona Kusini inakaliwa tena kwa mabavu kuliko kuwa na siku moja zaidi ya uhuru.

Kana kwamba Kusini si mali ya Lebanon, kana kwamba ni nchi tofauti kana kwamba Kusini si sehemu ya asili ya utamaduni wetu yenye utajiri wa historia unaopitia wakati mgumu.

Ni Kusini ambayo kimsingi inatuunganisha na Palestina. Wakati mmoja tulikuwa wamoja. Kwa wengi wetu, sisi bado ni wamoja.

Sasa ni majira ya kiangazi rasmi. Wakati watu matajiri wanamiminika kwenye vilabu vya ufuo vya Lebanon vilivyo na bei ya juu sana - hata ufikiaji wa ufuo umechukuliwa kutoka kwetu - wale ambao wanatumiwa vibaya na matajiri hao huingia kwenye bahari iliyochafuliwa kwa nguvu wakidhihaki ufuo wa Beirut, na wale walio katikati bado wanamiminika katika fukwa ya Sour bila malipo, licha ya vitisho vya kila siku, mabomu zaidi na vifo zaidi.

Walebanon si wastahimilivu - usituite hivyo - sisi ni wanadamu chini ya tishio la mara kwa mara la jirani bandia aliyewekwa kinyume cha sheria ambaye anataka kuharibu kila kitu tunachokithamini.

Na ni nani anayefurahia kuwazia maangamizi yetu - "Tutarudisha Beirut kwenye Enzi za Mawe," wanasema. Tunacheka na tunadhihaki: "Hatuna pesa, hakuna umeme, hakuna maji, tayari tuko katika Enzi ya Mawe, habibi."

Tunaweza kufanya nini?

Tunangojea yale yanayoweza kuepukika, tunawachukia watu wanaochochea vita, vyombo vya habari vya Magharibi na wanasiasa, Waisraeli wamwaga damu na washirika wao wakitamani kuangamia kwetu, huku tukiitazama Gaza, huku tukijaribu sana kufahamu kwa nini ulimwengu haitokoma kuuwa jamaa zetu, huku akili zetu zikizorota polepole lakini kwa kasi, huku tukijaribu kudumisha hali ya kawaida - tukijua kabisa kwamba hakuna jambo la kawaida kuhusu hili - huku tunaulizana "habari yako" wakati tunajua kikamilifu vizuri jibu ni nini.

Tunangoja tunapojaribu kujibu swali "je ni salama kuja Lebanon?" na wale walio nje ya nchi, ambao wanapaswa kufanya uamuzi mgumu wa kurudi na kutembelea wapendwa wao, na kuwa nao wakati vita vikubwa zaidi vinakaribia, labda kuzuka ("angalau tunakufa pamoja") au kuamua tushinde, ikiwezekana kulazimishwa kutazama matukio ya kutisha yanayotokea kwa mbali, kwa sababu vipi ikiwa uwanja wa ndege utapigwa kwa bomu na hawawezi kurudi kwenye maisha yao ya kawaida nje ya nchi, ambayo waliyafanyia kazi kwa bidii, ambayo yanawawezesha kuwatumia fedha zinazowezesha familia yao na sehemu kubwa ya Lebanoni kuendelea?

Hakuna njia ya kujua. Kuna hali tu ya kutisha ya kutokuwa na uhakika. Kuna vitisho tu na matakwa ya taifa la Israeli lenye itikadi kali za kijamii ambalo, kama tulivyoona, hufurahia kuleta mambo ya kutisha zaidi kufanywa na mwanadamu. Na kisha kulia na kuangazia ulimwengu kuwa anadhulumiwa.

Wakati huo huo, tunasubiri ili umeme urudi, na mwisho wa dunia.

AFP