zaidi ya watu 100 waliuawa katika mafuriko na maporomoko wa ardhi katika maeneo tofauti nchini Rwanda / Photo: AFP

Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Makazi nchini Rwanda, Noel Nsanzinenza anasema zaidi ya dola bilioni 25 za Marekani zinahitajika kujenga nyumba 3006 .

Hii ni kwa ajili ya walioathiriwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi .

Serikali inasema mnamo tarehe 2 na 3 Mei , watu 131 waliuawa katika maeneo yalioathiriwa Magharibi, Kaskazini na Kusini mwa Rwanda.

Baraza la mawaziri la Rwanda limeidhinisha mpango wa kukabiliana na dharura wa kuwasaidia wale walioathiriwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika baadhi ya maeneo ya nchi.

Ina lengo la kuimarisha juhudi za kutoa unafuu wa haraka kwa jamii zilizoathiriwa na kuziagiza taasisi zinazohusika kutekeleza mpango wa teknolojia bila kuchelewa.

“Baraza la Mawaziri linazitaka jamii katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko kutekeleza tahadhari na kuwa waangalifu zaidi, kwani mvua nyingi zaidi zinaweza kutarajiwa katika siku zijazo,” inasema taarifa ya maazimio ya mkutano wa mawaziri.

“Wananchi wanaombwa kuwa makini kwa maelekezo yanayotolewa na mamlaka za mitaa ikiwa ni pamoja na kudumisha viwango vya usafi na usafi wa mazingira ili kuzuia uwezekano wa milipuko ya magonjwa.”

Hela zinazohitajika

Rwanda inahitaji angalau Rwf 130 bilioni ($116.2 milioni) kukarabati miundombinu muhimu iliyoharibiwa wakati wa mafuriko, Waziri wa Usimamizi wa Dharura, Marie-Solange Kayisire alisema Jumamosi wakati wa Mkutano wa Mawaziri na waandishi wa habari katika mji mkuu Kigali.

Fedha hizo zitatumika kukarabati barabara, shule na vituo vya matibabu vilivyoharibiwa na mafuriko ya tarehe 2 na 3 Mei, na maporomoko ya ardhi yaliyogharimu maisha ya watu 131.

Zaidi ya nyumba 6,000 zilisombwa na mafuriko katika majimbo ya kaskazini, magharibi na kusini mwa Rwanda.

Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyotokea tarehe 3 na 4, inafikia 131, serikali ilisema.

TRT Afrika