Muwakilishi wa Marekani ndani ya Umoja wa Mataifa, akiwa mjini New York siku ya kupiga kura ya turufu kusitisha mashambulizi ya Israel dhidi ya mji wa Gaza. / Picha: Reuters  

Na Assal Rad

Baada ya kupinga maazimio matatu tofauti ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kutaka kusitishwa kwa mapigano huko Gaza, hatimaye Marekani imeshindwa kupiga kura katika azimio la hivi karibuni la kusitisha mapigano, na kuruhusu kupitishwa kwake.

Azimio hilo linaashiria mabadiliko katika msimamo wa Marekani na kuibua upinzani kutoka kwa Israel (Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu aliwazuia ujumbe uliopangwa kwenda Marekani baada ya Marekani kukataa kutumia mamlaka yake ya kura ya turufu mara ya nne. Lakini utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden haraka ulidhoofisha umuhimu wa azimio hilo.

Saa chache baada ya azimio hilo kupitishwa, msemaji wa Ikulu ya White House John Kirby alisema kuwa kutohusika kwa Marekani "hakumaanishi kuwepo mabadiliko katika sera zetu."

Na katika mkutano na waandishi wa habari, msemaji Matthew Miller alidai "ni azimio lisilofunga," huku akiweka wazi msimamo wa Marekani na kupendekeza kwamba azimio la kusitisha mapigano ni maoni ya chombo cha Umoja wa Mataifa, na sio sheria.

Katika mahojiano makali na Miller, mwanahabari wa Associated Press Matt Lee aliuliza swali ambalo waangalizi wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu vita vya Israel dhidi ya Gaza: "Nini maana ya Umoja wa Mataifa au Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa?"

Wataalamu na wachambuzi, kama vile afisa wa zamani wa Umoja wa Mataifa na mwanasheria wa haki za binadamu, Craig Mokhiber, walielezea ukosoaji wao kwa Marekani kwa kudhoofisha azimio hilo, ambalo tayari ni dhaifu, kwa kutoa wito wa "kusitishwa mapigano kwa mwezi wa Ramadhani" ambayo hatimaye kuleta suluhisho la kudumu."

Mokhiber aligonga vichwa vya habari Oktoba 2023 baada ya kujiuzulu kama mkurugenzi wa ofisi ya New York ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, akitaja kushindwa kwa Umoja wa Mataifa kuzuia "mauaji ya kimbari" huko Gaza.

Wakati hilo likipuuzwa, upitishaji wake ulipokelewa kwa shangwe na Umoja wa Mataifa kwa sababu ya haja kubwa ya kushughulikia mzozo wa kibinadamu huko Gaza, ambayo ni pamoja na kuongezeka kwa njaa ambayo haijapata kutokea, kulingana na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji David Miliband.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliweka wazi kwamba azimio hilo sio tu tamko lisilofunga, ni "lazima litekelezwe" na kushindwa kutekelezwa kwake hakutosameheka." Hata hivyo, alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo anadhani azimio hilo lingeifanya Israel kutangaza kusitisha mapigano, msemaji Miller alijibu, "Sidhani."

Hakuna shaka kwenye umuhimu wa kupitishwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa la kusitisha mapigano hayo. Inatoa msingi zaidi wa kisheria wa uwajibikaji wa Israeli juu ya hatua zake huko Gaza na uhalali wa kisheria kwa tuhuma za ushirikiano kwa baadhi ya nchi - kama Marekani - ambazo inaendelea kuunga mkono na kutuma silaha katika vita vya "mauaji ya kimbari" ya Israeli.

Kama ulivyo uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki wa mwezi Januari, azimio la Umoja wa Mataifa la kusitisha mapigano linaongeza nguvu kwenye ushahidi na wajibu wa kisheria wa Israel na wafuasi wake kusitisha vita dhidi ya Gaza, vita ambavyo tayari vimeua zaidi ya Wapalestina 32,000 huku maelfu ya watu wakiwa hawajulikani waliko.

Mmoja wa raia wa Palestina, akiomboleza vifo vya ndugu zake waliouwawa katika mashambulizi ya Israel yanayoendelea dhidi ya Gaza. (AFP/Mohammed Abed).

Wakati huo huo, wakosoaji wako sahihi kuhoji uhakika wa hatua hizi wakati ukweli wa azimio hilo haubadilishi hali halisi ya Wapalestina.

Israel imeendelea kupuuzia sheria za kimataifa kwa miongo kadhaa kutokana na kuendelea kukalia kwa mabavu ardhi ya Wapalestina, ubaguzi wa rangi, upanuzi wa makaazi na unyakuzi wa ardhi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, pamoja na kuzingirwa kwa Gaza, na kuruhusu ghasia dhidi ya Wapalestina, uhalifu wa kivita, na uhalifu mwingine.

Kwa sasa, Israel imechukuia sheria za kimataifa na haki za binadamu kwa kiwango kikubwa zaidi, huku matamshi yakiendana na vitendo ambavyo ni vya mauaji ya halaiki na vikwazo vyake vya makusudi vya kuzuia misaada kuingia Gaza, hivyo kusababisha njaa inayosababishwa na mwanadamu.

Kwa hivyo, ni nini maana ya Umoja wa Mataifa au Baraza la Usalama? Pamoja na kuundwa kwake baada ya Vita Vya Dunia vya pili, kanuni za msingi zaidi za Umoja wa Mataifa zilikuwa kulinda vizazi vijazo kutokana na janga la vita na kuhakikisha haki za kimsingi za binadamu kwa watu wa mataifa yote.

Ingawa shirika la kimataifa linaweza kutangaza sheria hizi na kupendekeza hatua zinazohitajika, uamuzi wa kuzitekeleza bado uko kwa mataifa yenyewe.

Wakati Israel yenyewe imeonesha kutojali kabisa mfumo wa kimataifa, ni wajibu wa mataifa mengine—hasa waungaji mkono na waungaji mkono wake—kuwawajibisha.

Mengi yanaweza kusemwa juu ya unafiki wa Magharibi na mapendeleo ambayo ni ya kawaida katika siasa za madaraka, lakini dharau wazi ambayo serikali ya Biden imeonyesha kwa mfumo wa kimataifa pamoja na kujivunia, ili kuifanya Israeli kuwa juu ya sheria, imepita mipaka ya unafiki.

Nia ya utawala wa Biden kuitenga Marekani kutoka jukwaa la kimataifa, na kuondoa uaminifu wake, na kimsingi kupuuza jumuiya ya kimataifa unaakisi hatari za sera za kigeni za Marekani.

Licha ya matamshi ya mashirika ya kimataifa kama vile Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya Duniani, na Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ushahidi wa wataalamu wa Umoja wa Mataifa, ushahidi kutoka kwa mashirika ya kimataifa ya misaada na haki za binadamu kama vile Madaktari Wasio na Mipaka, Oxfam International, na Human Rights Watch, na maelezo ya mashahidi wa waandishi wa habari na wafanyakazi wa misaada huko Gaza, Marekani inaendelea kutetea matendo ya Israel na kukana makosa yaliyotendwa na Israel.

Kwa kutumia Umoja wa Mataifa kama chombo cha ajenda yake ya kisiasa, badala ya chombo cha sheria na haki za kimataifa, Marekani imekifanya chombo hicho kukosa maana.

Nia ya utawala wa Biden kuitenga Marekani kutoka jukwaa la kimataifa, na kuondoa uaminifu wake, na kimsingi kupuuza jumuiya ya kimataifa unaakisi hatari ya sera za kigeni za Marekani.

TRT Afrika