Miili ya takriban watu 52 imeopolewa kutoka Mto Kongo baada ya mashua yao kupinduka mwishoni mwa wiki iliyopita, waziri wa jimbo alisema Jumatatu, akionya kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi na wengi bado hawajulikani.
Boti hiyo ilikuwa imebeba zaidi ya watu 300 ilipopinduka karibu na mji wa Mbandaka kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo usiku wa Ijumaa. Mwishoni mwa wiki 30 walithibitishwa kufa maji huku 167 wakipotea.
Didier Mbula, waziri wa afya wa mkoa wa Equateur, aliambia Reuters kwamba idadi ya waliofariki imeongezeka tangu wakati huo.
"Tumerekodi miili 52 ambayo ilopolewa. Timu za msako bado ziko uwanjani, zikifanya kazi. Hii bado ni iadai tu ya mwanzo, na inaweza kuongezeka zaidi," alisema kwa simu.
Siku ya Jumatatu, Waziri wa Uchukuzi Marc Ekila alisema mashua iliyopinduka haikupaswa kuabiri usiku, ilikuwa imejaa kupita kiasi, na haikutambua ipasavyo wamiliki wake au idadi ya abiria waliokuwemo.
Katika taarifa yake, aliahidi kutekeleza sheria za kuboresha usalama wa usafiri wa mtoni na "kupunguza majanga yanayotokea mara kwa mara."