Rais wa Congo, Felix Tshisekedi/ Photo: AA

Hotuba hiyo ililitolewa wakati wa mkutano kati ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na mwenzake wa Uswizi, Rais Alain Berset katika ziara ya siku tatu nchini DRC.

Walijadili hasa ukosefu wa usalama huko Mashariki mwa DRC.

Rais wa DRC alisisitiza kwa mara nyingine tena kwamba hakuna suala la mazungumzo yoyote ya kisiasa na wavamizi wa taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambao wanatishia utalii nchini .

"Hakuna suala la mazungumzo ya kisiasa na kundi hili. Ninasema na nataka niweke wazi, hakutakuwa na swali lolote kuhusu hilo'' Rais wa DRC anaongeza kuwa kila kitu kimewekwa katika hatua ili kuharakisha mchakato wa kuwapokonya silaha, kuwaondoa na kuwajumuisha tena wale wapiganaji wa M23 ambao watathibitisha utaifa wao kwa Congo'' alikiri rais Tshisekedi.

Katika chapisho kwenye mtandao wao wa Twitter, M23 walijibu kwa kuweka masharti ya mazungumzo ya moja kwa moja ya kisiasa kati yao na serikali juu ya kukubali kuondoka katika vijiji huko DRC, kupokonywa silaha na kusaliti amri.

''Mradi tu hakuna mazungumzo ya moja kwa moja ya kisiasa kati ya M23 na serikali ya Kinshasa, pia hakutakuwa na utatuzi, upokonyaji silaha na uondoaji silaha'' anasema Lawrence Kanyuka, msemaji wa kisiasa wa M23.

Kwa yale yanayohusu mamlaka ya jeshi la kanda ya EAC, rais wa DRC anathibitisha kwamba baada ya kuhamishwa kwa M23 katika mji wa Kindu, huko Maniema, ''haitakuwa muhimu kuweka kikosi cha EAC nchini Kongo'' alithibitisha tena Rais Tshisekedi.

TRT Afrika