Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, amesema kuwa serikali ya nchi hiyo itahakikisha kuwa ugonjwa wa Ebola hauingii nchini Marekani.
“Kwa bahati mbaya Shirika la Afya Duniani halijafanya jitahada za kutosha kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo hadi kufikia sasa kama walivyoshindwa wakati wa UVIKO 19,” alisema Rubio siku ya Alhamisi.
ZILIZOPENDEKEZWA
Kauli ya Rubio inakuja wakati Marekani imesitisha utoaji viza kwa raia wanaotokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) kwa hofu ya ugonjwa wa Ebola.
Pia, inakuja wakati dadi ya vifo vilivyotokana na ugonjwa huo, ikifikia 139 kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).
CHANZO:AA
















