| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Wanajeshi saba wa Nigeria wauawa katika shambulio la kigaidi
Wanajeshi wasiopungua saba waliuawa mwishoni mwa wiki katika shambulio linaloshukiwa kuwa la kigaidi kaskani magharibi karibu na mpaka wa Niger.
Wanajeshi saba wa Nigeria wauawa katika shambulio la kigaidi
Wanajeshi wa Nigeria wasiopungua saba wameuawa katika mashambulizi ya kigaidi katika jimbo la Sokoto. / Reuters

Wanajeshi wa Nigeria wasiopungua saba wameuawa mwishoni mwa wiki katika shambulio la kigaidi kaskazini magharibi karibu na mpaka wa Niger, vyanzo vya kijeshi na eneo hilo vilisema Jumanne.

Vikosi hiyo viliuawa Jumamosi usiku wakati gari lao lilipoharibika walipokuwa wanarudi kutoka katika operesheni katika kambi ya kundi la kigaidi ya Lakurawa nje ya eneo la Illela jimbo la Sokoto.

Lakurawa, ambayo ina uhusiano na magaidi wa eneo la Sahel, ipo katika majimbo ya Kebbi na Sokoto kaskazini magharibi mwa Nigeria 2018 na imekuwa ikiendesha shughuli zake tangu 2023.

Jeshi la Nigeria lilithibitisha mashambulizi hayo ingawa halikutowa idadi ya waliouawa.

'Masikitiko kwa wanajeshi kuuawa'

"Kwa masikitiko makubwa wanajeshi wameuawa mwishoni mwa wiki karibu na Illela," Luteni Kanali Olaniyi Osoba, msemaji wa jeshi katika kanda hiyo, aliiambia AFP.

"Hata hivyo, wanajeshi zaidi walipelekwa katika eneo hilo," alisema, akiongeza kuwa operesheni inaendelea ya "kuwasaka na kuwakata makali magaidi waliohusika."

Vyanzo viwili vilithibitisha kuwa wanajeshi saba waliuawa wakati wakitengeneza gari lao.

Mashambulizi ya Jumamosi yametokea siku ambayo Marekani na Nigeria walisema wamemuua Abu Bilal Al Manuki, naibu kiongozi wa Daesh, katika mashambulizi ya pamoja ya angani kwa kambi zake kanda ya Ziwa Chad.

Al Manuki, raia wa Nigeria, alifuatiliwa hadi kwenye maficho yake kijiji cha mbali cha Metele karibu na mpaka wa Niger kupitia simu yake ya satelaiti, chanzo cha kijasusi cha Nigeria kiliiambia AFP.

CHANZO:TRT Afrika Swahili