| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Rais Mwinyi aishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuipatia misaada ya maendeleo Zanzibar
Rais Mwinyi amesema misaada hiyo imeleta mabadiliko chanya katika sekta za elimu, afya na miundombinu.
Rais Mwinyi aishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuipatia misaada ya maendeleo Zanzibar
Rais Mwinyi amesema misaada hiyo imeleta mabadiliko chanya katika sekta za elimu, afya na miundombinu. / TRT Afrika Swahili

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuipatia Zanzibar misaada ya maendeleo inayochangia ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii.

Rais Mwinyi amesema misaada hiyo imeleta mabadiliko chanya katika sekta za elimu, afya na miundombinu, huku akiitaka Benki hiyo kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha huduma za afya, nishati ya uhakika pamoja na miradi ya maendeleo ikiwemo BIG Z.

Ameyasema hayo alipokutana na aliyekuwa Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia Kanda ya Tanzania, Malawi, Zimbabwe na Zambia Nathan Belete, aliyefika Ikulu kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini pamoja na kumtambulisha Mkurugenzi Mpya, Firas Raad.