Mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umewauwa zaidi ya watu 80 huku mamlaka ikionya kuwa hakuna chanjo ya aina hiyo katika mlipuko ambao Shirika la Afya Duniani lilitangaza dharura ya kimataifa ya afya siku ya Jumapili.
Jumla ya vifo 88 na maambukizi 336 vinavyoshukiwa kuwa na homa inayoambukiza sana ya kuvuja damu vimeripotiwa, Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC Africa) vilisema katika ripoti mpya Jumamosi.
WHO yenye makao yake Geneva ilisema mlipuko uliosababishwa na aina ya Ebola ya Bundibugyo ulikuwa "dharura ya afya ya umma ya wasiwasi wa kimataifa". Hicho ni kiwango cha pili cha juu cha tahadhari chini ya kanuni za afya za kimataifa.
Shirika la afya ulimwenguni lilionya kiwango halisi cha idadi ya maamukizi na kuenea haikuwa wazi lakini iliacha kutangaza dharura ya janga, kiwango cha juu zaidi cha tahadhari kilichoanzishwa mnamo 2024.
'Hakuna chanjo, hakuna tiba'
Kundi la misaada ya kimatibabu la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) lilisema lilikuwa linatayarisha "hatua za dharura ", likiita kuenea kwa kasi kwa mlipuko huo "kutia wasiwasi sana", katika maonyo yaliyosisitizwa na mamlaka.
"Aina ya virusi vya Bundibugyo havina chanjo, havina tiba mahususi," Waziri wa Afya wa DR Congo, Samuel-Roger Kamba alisema.
"Aina hii ina kiwango cha juu sana cha vifo, ambacho kinaweza kufikia 50%.
Ugonjwa huo, ambao uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2007, pia umemuua raia wa Congo katika nchi jirani ya Uganda, maafisa walisema Jumamosi.
Chanjo zinapatikana tu kwa aina ya Zaire, ambayo ilitambuliwa mwaka wa 1976 na ina kiwango cha juu cha vifo cha 60-90%.
Maafisa wa afya walithibitisha mlipuko wa hivi karibuni Ijumaa katika mkoa wa Ituri kaskazini-mashariki mwa DRC, unaopakana na Uganda na Sudan Kusini, kulingana na CDC Afrika.















