| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Iran yatangaza bodi mpya ya kusimamia Mlango Bahari wa Hormuz
Udhibiti wa Iran wa njia hiyo ya baharini umetatiza soko la dunia na kuwapa uwezo muhimu, huku Marekani ikiweka vizuizi vyao vya baharini kwa bandari za Iran.
Iran yatangaza bodi mpya ya kusimamia Mlango Bahari wa Hormuz
Wakati wa amani, humusi ya mafuta na gesi ulimwenguni hutumia njia hiyo. / Reuters

Taasisi ya juu ya usalama ya Iran imetangaza Jumatatu kuundwa kwa bodi mpya itakayosimamia Mlango Bahari wa Hormuz, ambao Iran umeufunga na inataka kutoza meli ambazo zinautumia.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X, Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa limeweka ujumbe kwa Mamlaka ya Mlango Bahari wa Ghuba (PGSA) ukisema litatoa "taarifa za moja kwa moja kuhusu (#Hormuz_Strait operations) na yale yanayojiri."

Akaunti ya Jeshi la Mapinduzi la wanamaji pia ilisambaza ujumbe huo.

Haikufahamika majukumu ya bodi hiyo mpya yatakuwa yapi lakini mapema mwezi huu Televisheni ya Iran yenye kutangaza kwa Kiingereza Press TV ilisema kumeundwa "mfumo wa kuwa na uhuru juu ya Mlango Bahari wa Hormuz" na kwamba meli zinazopita katika Mlango Bahari huo zimetumiwa "utaratibu" kutoka kwa barua pepe ya info@pgsa.ir.

Kwa sehemu kubwa Iran imekuwa ikizuia meli kupita kwenye mlango bahari huo muhimu tangu kuanza kwa vita na Marekani na Israel Februari 28. Mapigano yamesitishwa tangu Aprili 8.

Udhibiti wa Iran wa njia hiyo ya baharini umetatiza soko la dunia na kuwapa uwezo muhimu, huku Marekani ikiweka vizuizi vyao vya baharini kwa bandari za Iran.

Wakati kukiwa na amani, humusi ya mafuta na gesi ulimwenguni hutumia njia hiyo, pamoja na bidhaa zingine muhimu ikiwemo mbolea.

Tangu kuanza kwa vita, Iran imekuwa ikisema kuwa hali katika mlango bahari huo "haitorudi kuwa kama ilivyokuwa kabla ya vita" na mwezi uliopita ilisema imepokea matozo ya kwanza kutokana na kutumiwa kwa njia hiyo ya bahari.

Siku ya Jumamosi, Ebrahim Azizi, mkuu wa tume ya usalama wa taifa ya bunge, alisema Iran "imeandaa mfumo wa kitaalamu wa kuongoza usafiri wa meli" katika mlango bahari huo, akiongeza kuwa "utazinduliwa karibuni".

CHANZO:TRT Afrika Swahili