Mwanamke huyo ambaye pia alikuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili alifariki dunia alipokuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi kutokana na majeraha ya moto yaliyodaiwa kusababishwa na kumwagiwa na petroli katika eneo la Mwiki, Kasarani.
Kisa hicho kilizua mshtuko mkubwa nchini Kenya na kuamsha mjadala kuhusu ongezeko la ukatili dhidi ya wanawake pamoja na chuki zinazohusishwa na siasa.
Rachel alikuwa gumza mitandaoni baada ya kuonyesha tattoo za Rais Ruto pamoja na ujumbe wa kumuunga mkono kisiasa. Wakati baadhi ya watu walimsifu kwa uaminifu wake wa kisiasa, wengine walimkosoa vikali na kumshambulia kwa maneno mtandaoni.
Idara ya Polisi imesema uchunguzi kuhusu shambulio hilo unaendelea. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kipchumba Murkomen, alimtembelea Wandeto hospitalini kabla ya kifo chake na kulaani shambulio hilo, akielezea kama "kitendo cha woga na kisicho cha kibinadamu."
Hadi sasa hakuna aliekamwata kuhusiana na shambulio hilo. Aidha, uchunguzi bado unaendelea ili kubaini kama shambulio hilo lilihusiana moja kwa moja na matamshi yake ya kisiasa au lilitokana na nia nyingine.













