Marekani na Israel walikuwa na mpango wa kumuweka madarakani rais wa zamani wa Iran na mwenye msimamo mkali siku chache baada ya nchi mbili hizo kuanzisha mashambulizi dhidi ya Iran na kumuua aliyekuwa kiongozi mkuu Ali Khamenei, hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Jumanne ya gazeti la The New York Times.
Maafisa wa Marekani wameiambia The Times kuwa mpango huo ulibuniwa na Israel kwa kupitishwa na Marekani ili kubadilisha utawala wa nchi hiyo, baada ya Rais Trump kupendekeza siku za mwanzo za mapigano kwamba: itakuwa vyema iwapo "miongoni mwao" Iran atachukua madaraka ya nchi.
Kwa mujibu wa gazeti la The Times, "mtu" huyo alikuwa ni Mahmoud Ahmadinejad, "aliyekuwa rais wa Iran anayejulikana kwa msimamo mkali dhidi ya Israel na Marekani," ambae inaripotiwa alishauriwa kuhusu mabadiliko ya utawala mpya.
Taarifa ya gazeti la The Times inasema haifahamiki ni kwa namna gani Ahmadinejad alichaguliwa, ikizingatiwa kwamba msimamo wake unafahamika wakati wa uongozi wake kuanzia 2005-2013 na wito wake wa kutaka "kuifuta Israel katika ramani."
Pia ni muungaji mkono mkubwa wa mpango wa nyuklia wa Iran, mkosoaji mkubwa wa Marekani.
Hata hivyo, mpango huo uliharibika baada ya Ahmadinejad "kujeruhiwa siku ya kwanza ya mashambulizi ya Israel yaliyolenga nyumba yake mjini Tehran ambayo yalikuwa na lengo la kumuacha huru kutoka kifungo cha nyumbani," kwa mujibu wa maafisa waliozungumza na The Times.
Gazeti la Times limeripoti kwamba Ahmadinejad, ambae awali alisalimika katika shambulizi, hajaonekana hadharani tangu muda huo na kwamba Marekani haina taarifa ya alipo au hali yake ya kiafya.



















