| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mbunge wa zamani wa Ghana ajeruhiwa kwa risasi nyumbani kwao
Maafisa kutoka Idara ya Ujasusi waliitikia wito wa kutoa msaada kutoka katika nyumba hiyo na kuanzisha uchunguzi.
Mbunge wa zamani wa Ghana ajeruhiwa kwa risasi nyumbani kwao
Mbunge wa zamani Sarah Adwoa Safo alijeruhiwa baada ya walinzi kufyatua risasi wakilenga gari lake. / Wengine

Mbunge wa zamani wa eneo bunge la Dome-Kwabenya Sarah Adwoa Safo alijeruhiwa kwa risasi iloshambulia gari lake wakati akitembelea nyumba ya marehemu baba yake eneo la, jijini Accra.

Kulingana na polisi, mbunge huyo wa zamani alipata majeraha ya risasi katika sikio lake la kushoto kwa shambulizi hilo la Jumapili, Juni 21. Gari lake pia lilikuwa na ishara ya kushambuliwa kwa risasi.

Taarifa kutoka Idara ya Polisi ya Ghana zinasema shambulio hilo lilitokea punde tu Adwoa Safo alipowasili nyumbani hapo, ambapo kulikuwa na sherehe.

“Polisi wanachunguza tukio la walinzi wa eneo hilo wenye silaha kufyatua risasi katika nyumba hiyo, kusababisha jeraha kwa Mheshimiwa Adwoa Safo. Gari lake pia lilipatikana na ishara za risasi ,” polisi walisema katika taarifa.

Uchunguzi umeanzishwa

Maafisa kutoka Idara ya Ujasusi waliitikia wito wa kutoa msaada kutoka katika nyumba hiyo na kuanzisha uchunguzi.

Polisi nchini Ghana wamewakamata walinzi sita kuhusiana na tukio hilo la kushambulia risasi.

Shambuli hilo limesababisha wasiwasi tena kuhusu usalama wa wanasiasa nchini Ghana. Nchi hii imekumbwa na matukio ya vurugu yakihusisha wanasiasa katika miaka kadhaa, ikiwemo mauaji ya mbunge wa zamani wa eneo bunge la Hayford Ekow Quansah 2020 aliposhambuliwa na watu wenye silaha wakati wa kampeni za uchaguzi.

Polisi wanasema uchunguzi kuhusu tukio hilo la kufyatuliwa risasi kwa Kwabenya unaendelea.

CHANZO:TRT Afrika English