Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan alilakiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa ziara rasmi nchini Urusi.
Kulingana na vyanzo vya kidiplomasia vya Uturuki, Putin alimlaki Fidan katika mji wa Urusi wa Kazan.
Taarifa ya mazungumzo katika mkutano huo ilitolewa na Kremlin, ambapo walimnukuu Putin akisema kuwa ushirikiano kati ya Urusi na Uturuki "unaimarika vizuri."
"Tumefurahi sana kuhusu hatua hii," Putin alisema katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov na mshauri wa rais Yury Ushakov.
Putin alisema mawasiliano kati ya nchi hizo mbili siyo tena rasmi na badala yake yamekuwa ya "kirafki zaidi, na kuimarika kila siku."
Kremlin yapongeza nafasi ya Erdogan
Alisema kuwa hii zaidi ni kutokana na msimamo uliochukuliwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, na kumuomba Fidan amfikishie salamu zake, pamoja na kueleza kuwa amefurahi kumuona nchini Urusi.
"Nimefurahi kupata fursa ya kukutana na wewe pembeni mwa mkutano mkuu na kujadili masuala ya maslahi ya pamoja yanayojiri kwa mataifa yetu yote mawili," Putin aliongeza.
Fidan alimpa Putin "salamu za dhati" za Erdogan, na kuongeza: "Kwa hakika, eneo letu na dunia kuna agenda nyingi za kimataifa, na uzoefu wako katika suala hili ni muhimu. Kuna masuala mengi ambayo tunahitaji kujadili."












