Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amemlaki Waziri Mkuu wa Singapore Lawrence Wong katika hafla fupi iliyofanyika jijini Istanbul siku ya Ijumaa, kabla ya viongozi hao kufanya mazungumzo.
Hafla hiyo ilifanyika katika jumba la Rais la Dolmabahce, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Wong nchini Uturuki.
ZILIZOPENDEKEZWA
Muda mfupi baadaye, viongozi hao wawili, walikuwa na mazungumzo yaliyolenga ushirikiano wa nchi hizo mbili.
Kati ya waliohudhuria mazungumzo hayo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan, Waziri wa Fedha Mehmet Simsek, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Burhanettin Duran, Mshauri Mwandamizi wa Rais wa Masuala ya Usalama na Sera ya Nje Akif Cagatay Kilic.
CHANZO:AA












