Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech Andrej Babis, amesema kuwa sheria mpya yenye kupiga marufuku matumizi ya simu za mikononi mashuleni, itaanza kufanya kazi mwezi Septemba 2027.
Kupitia picha mjongeo iliyowekwa kwenye ukurasa wa X, Babis alisema kuwa wamefikia makubaliano na Waziri wa Elimu Robert Plagaon, kuhusu kanuni ya kudhibiti matumizi ya simu za mikononi mashuleni.
Kulingana na Waziri Mkuu huyo, sheria hiyo itapiga marufuku matumizi ya simu za mikonono madarasani.
Sheria hiyo, itaendelea kufanya kazi hata wakati wa mapumziko.
Kwa sasa, ndani ya Jamhuri ya Czech, uamuzi wa kutumia simu hizo unabakia kwenye ngazi ya shule na si vinginevyo.
CHANZO:AA









