Idadi ya vifo vya Wapalestina inaongezeka / picha: AA

Kanisa la Anglikana huko Jerusalem limesema, Israel iliutaka uongozi wa hospitali ya Gaza 'mara tatu' kuondoka siku chache kabla ya shambulio baya katika Hospitali ya Al Ahli Arab huko Gaza kutokea.

“Tulipokea maagizo matatu ya kuondoka katika eneo la hospitali, Jumamosi, Jumapili, na Jumatatu. Hospitali ililipuliwa Jumanne," Askofu Mkuu wa Anglikana Hosam Naoum alisema.

"Maagizo kadhaa yalitolewa kwa njia ya simu," madai ya askofu Mkuu Naoum yanadhoofisha madai ya Israeli kwamba mlipuko uliosababisha mauaji ya zaidi watu 500 katika hospitali hiyo yametokana na roketi zenye hitilafu za Islamic Jihad.

Israel inasema vifo vya wanajeshi wake vimeongezeka hadi 306

Jeshi la Israel limesema vifo vya wanajeshi wake katika mzozo wa sasa na makundi ya Wapalestina vimeongezeka na kufikia 306.

Picha:AFP

Jeshi lilitangaza majina ya maafisa wawili wa ziada wa usalama na askari wa akiba waliouawa katika mapigano karibu na mpaka na Gaza katika taarifa ya mtandaoni siku ya Alhamisi.

Wizara ya Afya ya Israel inasema kuwa Waisraeli 4,629 wamejeruhiwa na wengine 1,400 wameuawa huku mamlaka ya afya huko Gaza ikirekodi vifo 3,478 na majeruhi zaidi ya 13,000 kufikia Oktoba 18.

China 'imesikitishwa sana' na Marekani kupinga azimio la Umoja wa Mataifa

China inasema 'imesikitishwa sana' na Marekani kupinga azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Israel na Hamas China.

Inasema, "imesikitishwa sana" na uamuzi wa Marekani wa kupinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka "kusitishwa kwa msaada wa kibinadamu" katika mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema China imesikitishwa sana na hatua ya Marekani ya kuzuia Baraza la Usalama kupitisha rasimu ya azimio kuhusu suala la Palestina."

Urusi kuwasilisha tani 27 za misaada ya kibinadamu huko Gaza

Urusi imetangaza mapema kuwa inapeleka tani 27 za misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Gaza huku kukiwa na mzozo unaoendelea katika eneo hilo.

Taarifa ya Wizara ya Hali ya Dharura ya nchi hiyo kwenye Telegram ilisema kwamba ndege maalum ilipaa kutoka Moscow kuelekea uwanja wa ndege wa El-Arish katika Peninsula ya Sinai nchini Misri, ikiwa imebeba unga, sukari, mchele na pasta.

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanasema halki inazidi kuzorota katika maeneo ya Gaza/ Picha AA

"Misaada ya kibinadamu ya Urusi itakabidhiwa kwa wawakilishi wa Jumuiya ya Nyota Nyekundu ya Misri kwa ajili ya kupelekwa katika Ukanda wa Gaza," taarifa hiyo iliongeza.

Shambulio la anga la Israel lapiga makazi ya raia

Wapalestina kadhaa wameuawa kutokana na shambulizi la anga la Israel kwenye nyumba iliyo karibu na shule inayohifadhi watu waliokimbia makazi yao kusini mwa Gaza.

Ndege za kivita za Israel zilishambulia nyumba karibu na Shule ya Ahmed Abdelaziz inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina Mashariki ya Karibu (UNRWA), katika kambi ya wakimbizi ya Khan Younis.

Hii ni kwa mujibu wa Shirika rasmi la habari la WAFA.

Imesema takriban Wapalestina tisa waliuawa, wakiwemo watoto saba, katika shambulio la anga la Israel kwenye nyumba ya familia ya Al Bakri na kuongeza kuwa, kuna wanafamilia bado wapo chini ya vifusi.

TRT Afrika