Polisi walikuwepo eneo la mkasa. Picha: AP

Ripoti za awali zinaonyesha kuwa watu kadhaa waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Watu kumi walipelekwa hospitalini na polisi, na wengine 19 walikwenda hospitali wenyewe.

Kituo cha Marekani cha Fox 45 kinaongeza kuwa shahidi alisema alisikia milio ya risasi 20 hadi 30.

Polisi wa Baltimore hawakutoa idadi kamili ya walioumia au kupigwa risasi mara moja au maelezo kuhusu utambulisho wa aliyefyatua risasi.

Alisema ufyatuaji risasi ulifanyika katika mtaa wa 800 wa Gretna Avenue ambapo mamia ya watu walikuwa wamefika kuhudhuria hafla inayoitwa "Brooklyn Day".

Reuters