Vikundi vya watu wa asili waandamana Sao Paulo dhidi ya muswada wa kudhibiti haki za ardhi

Vikundi vya watu wa asili waandamana Sao Paulo dhidi ya muswada wa kudhibiti haki za ardhi

Watu wa asili walikusanyika Sao Paulo Jumapili (Juni 4) kuandamana dhidi ya muswada wa kupunguza haki zao za ardhi.
Zaidi ya makabila 300 tofauti yanayoishi kwenye maeneo 730 wanayoyachukulia kama ardhi ya asili, haswa katika msitu wa mvua wa Amazon | Picha: Reuters

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, wanachama kutoka jamii 16 za watu wa asili walitembea Sao Paulo kuandamana dhidi ya muswada wa PL 490, ambao unakataza kutambuliwa kwa ardhi za watu wa asili ambazo hazikuwa zimekaliwa wakati Katiba ya Brazil ilipotungwa mwaka 1988, kifungu kinachojulikana kama "kipindi cha wakati".

Mashauri ya kutambua ardhi za makabila pia yanachunguzwa na Mahakama Kuu.

Ingawa muswada huo, ambao ulipitishwa na Bunge mnamo Mei 30, hautaathiri maeneo yaliyotambuliwa kwa sasa, unaweza kuathiri maeneo mamia yanayosubiri tathmini.

Hatua hiyo ilionekana na wanaharakati wa mazingira na haki za binadamu kama kurudi nyuma baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa kundi la wakulima.

Zaidi ya makabila 300 tofauti yanayoishi kwenye maeneo 730 wanayoyachukulia kama ardhi ya asili, haswa katika msitu wa mvua wa Amazon.

Muswada huo bado unahitaji idhini ya Baraza la Seneti na saini ya Rais Luiz Inacio Lula da Silva. Anaweza kupiga kura turufu lakini huenda ikawa na uungwaji mkono wa kutosha katika Bunge kwa kuzipa kisogo kura turufu hizo.

Reuters