Kwa sasa kuna zaidi ya Waafrika wanaotafuta hifadhi 30,000 wanaoishi Israel, wengi wao ni vijana wa kiume na kulingana na ripoti za vyombo vya habari. / Picha: AP

Hamas imejibu ripoti za vyombo vya habari kuhusu Israel kuwaajiri Waafrika wanaotafuta hifadhi kupigana vita vyake dhidi ya Gaza kwa mvuto wa vibali vya kudumu vya ukaazi.

Kundi la Muqawama wa Palestina katika taarifa yake Jumapili kwenye kanali yake ya Telegram lilisema: "Jeshi la uvamizi la kigaidi linalowaajiri Waafrika wanaotafuta hifadhi kupigana huko Gaza ndani ya safu zao, kwa kubadilishana na kuwezesha kupata vibali vya ukaazi, ni uthibitisho wa kina cha utovu wa maadili."

"Shirika mbovu linakiuka sheria za msingi zaidi za haki za binadamu kwa kutumia hitaji la wahamiaji na wanaotafuta hifadhi kuwatupa vitani na kujaribu kufidia hasara kubwa ya idadi ya jeshi lake iliyosababishwa na upinzani wetu shupavu huko Gaza."

Hamas ilitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kulaani vitendo hivyo na kuiwajibisha Israel kwa ukiukaji huo mkubwa.

Kwa sasa kuna zaidi ya Waafrika wanaotafuta hifadhi 30,000 wanaoishi Israel, wengi wao ni vijana wa kiume na kulingana na ripoti za vyombo vya habari, mamlaka ya ulinzi ya Israel iliona wanaweza kuinua hamu ya waomba hifadhi ya kupata hadhi ya kudumu nchini Israel kama kichocheo.

TRT World