Martin Griffiths,  Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu / Picha: Reuters

Martin Griffiths, Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Kibinadamu anasema usaidizi unaotakikana hauingii Gaza.

"Milipuko ya mabomu Gaza inaendelea na inazidi kuwa mabaya hata katika maeneo yanayodhaniwa kuwa nisalama," amesema katika taarifa yake na kuongeza, "Misaada haiwafikiI waathiriwa licha ya juhudi zetu zote."

"Ulimwengu wenyewe unashindwa kukidhi haki za kibinadamu," ameongezea.

Grffiths aliyasema hayo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baraza la Usalama huku ukijadiliana na serikali ya Israeli kuhusu namna bora ya kuingiza mafuta Gaza, ambapo kuna lita 400,000 katika magari zinazosubiri kuingia Gaza.

"Iwapo tunataka kuzuia kuongezeka kwa janga hili la kibinadamu, mazungumzo lazima yaendelee - ili kuhakikisha vifaa muhimu vinaweza kuingia Gaza kwa kiwango kinachohitajika, kuwaokoa raia na miundombinu wanayoitegemea," aliongezea.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Watoto UNICEF, limesema kuwa dawa kidogo ambazo zimeweza kuingizwa Gaza na Umoja wa Mataifa zimeokoa maisha ingawa bado kuna mahitaji makubwa.

Lakini umesisitiza umuhimu wa kuruhusiwa kuingizwa kwa mafuta.

" Idadi ya vifo itaongezeka kwa kasi ikiwa hospitali hazina umeme wa kufanya kazi na ikiwa watoto wataendelea kunywa maji yasiyo salama," UNICEF imesema katika mtandao wake wa X.

TRT Afrika