Jumla ya maseneta na waakilishi  538 wanaopigiwa kura kutoka kila jimbondio watakayemchagua Rais/ Picha Reuters 

Novemba 5 2024 Wamarekani zaidi ya milioni mia mbili arobaini wanapiga kura kumchagua rais atakaye ongoza kwa miaka minne ijayo.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris na rais wa zamani Donald Trump wanapambana ana kwa ana katika kile kinachotazamiwa kuwa ushindani wa karibu zaidi katika historia ya uchaguzi wa Marekani.

Lakini tofauti na uchaguzi unavyofanyika katika demokrasia nyingi duniani, Wamarekani hawamchagui Rais moja kwa moja kupitia kura zao.

Wanatumia mfumo wa ''Electoral college.''

Chini ya Katiba ya Marekani, waanzilishi wa Marekani waliweka kwamba kila moja ya majimbo 50 yangefanya uchaguzi wake wa rais.

Chini ya mfumo tata wa Chuo cha wapiga kura, kila jimbo lina idadi fulani ya "electors ambao tutawaita wajumbe maalum wa kura," wanaogawanywa kulingana na idadi ya watu. Majimbo mengi yana mfumo kuwa chama kitakachopata kura nyingi kinatwaa viti vyote vya wajumbe vilivyotengewa jimbo hilo.

Kwa hiyo tarehe tano watu wanapiga kura kuwachagua wajumbe 538 ambao ndio watakao mchagua rais.

Kwanini wajumbe 538?

Hii ni jumla ya maseneta na waakilishi wanaopigiwa kura kutoka kila jimbo.

Idadi hii imegawanywa hivi: Maseneta 100 kutoka majimbo yote 50, kumaanisha maseneta wawili kutoka kila jimbo. Na waakilishi ambao wengine kwetu tunawaita wabunge 435 kutoka majimbo yote 50. Na hapa ndipo utasikia kila jimbo limetengewa idadi yake rasmi ya waakilishi kulingana na idadi ya watu wake, ilimradi wote wakijumlishwa wanatakiwa wafike 435. Washington, ambayo sio jimbo rasmi, pi aimetengewa viti vitatu vya wajumbe.

Na ili mtu ashinde Urais, anatakiwa kunyakua wajumbe 270 au zaidi kati ya jumla ya 538 walioko kutoka majimbo yote 50.

Na mara nyingi, ili hili litokee, matokeo kutoka majimbo yanayoitwa Swing states hutegemewa zaidi. Haya ni majimbo ambayo kawaida hayana msimamo thabiti na huenda yakampigia kura mgombea yeyote aliyewashawishi zaidi. Kwa hiyo ni vigumu kubashiri watapiga kura vipi.

Mwaka huu, kuna majimbo saba yanayotazamiwa kuwa swing states:

Pensylvania - Viti 19.

Georgia - Viti 16

North Carolina - viti 16

Michigan - Viti 15

Arizona - Viti 11

Wisconsin - Viti 10

Nevada - Viti 6.

Kamala Harris na Donald Trump, mbali na sera za ndani ya nchi, wamejikuta kwa kiasi kikubwa wakitetea sera zao juu ya Israel ambazo inasemekana ndicho kimesababisha mgawanyiko mkubwa katik auchaguzi wa mwaka huu kwa pande zote za Democrats na Republican.

Japo Wote wawili wameonekana kuunga mkono uundwaji wa serikali mbili za Palestina na Israel ili kutatua mzozo huo, wote wawili wameshikilia kusimama na Israel kufa kupona, na wengi wanasubiri kuona, atakayeingia Oval Office, je Atakuwa na ushawishi wowote au nia ya kweli kuzima mgogoro huo wa kwa kuwezesha uundwaji wa serikali mbili au ni pang’ang’a za kampeni tu?

TRT Afrika