Mtumbuizaji huyo wa opera wa Afrika Kusini 38, amezolea sifa baada ya onyesho la nguvu la pekee katika sherehe za kutawazwa kwa Mfalme Charles III huko Westminster Abbey.
Yende, mwimbaji wa soprano, ndiye Mwafrika wa kwanza kutumbuiza katika sherehe za kutawazwa kwa Waingereza. Alitumbuiza "Moto Mtakatifu", utunzi mpya wa mtunzi wa kitambo na filamu Sarah Class, mbele ya umati uliojumuisha wafalme na viongozi wa kimataifa.
Amepata pongezi nyingi kutoka kwa mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii baada ya utendaji wake.
Opera daima imekuwa kipenzi cha Mfalme Charles, ambaye amefanywa msimamizi wa zaidi ya mashirika kadhaa ya muziki ulimwenguni. Mnamo 1981, katika harusi yake mwenyewe na marehemu Princess Diana, Kiri Te Kanawa, mwimbaji wa opera kutoka New Zealand, aliimba.
Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Mfalme Charles kumtazama Yende akitumbuiza aliposikia sauti yake maridadi kwenye tamasha la maadhimisho ya miaka 75 ya Royal Philharmonic Orchestra, lililofanyika Windsor Castle mnamo Aprili 2022.
Hapo awali Yende alikuwa ameambia vyombo vya habari vya ndani kuhusu furaha yake ya kutazamwa na familia yake nyumbani pamoja na mamilioni ya watu ambao watafuata sherehe ya kutawazwa kote ulimwenguni.
Malkia wa muziki wa afro-pop wa Nigeria, Tiwa Savage atatumbuiza kwenye tamasha la kutawazwa kwa Mfalme Charles III siku ya Jumapili tarehe 7 Mei 2023 kwenye kasri ya Windsor, London.
Savage, 43, mwimbaji na mtunzi ambaye pia ana uraia wa Uingereza, atatumbuiza pamoja na watu mashuhuri wenye uzani mzito akiwemo Steve Winwood, DJ Pete Tong, Lang Lang, Lucy, Paloma Faith, na Olly Mur.
Mwaliko wake wa kutumbuiza kwenye kutawazwa ni hatua muhimu, kwani anakuwa msanii wa kwanza wa Nigeria kupokea heshima hiyo.