Mamlaka ya eneo la Gaza imeishutumu Israeli kwa kuiba viungo kutoka kwa miili ya Wapalestina na kuitisha uchunguzi wa kimataifa juu ya suala hilo.
Ofisi ya mawasiliano ya serikali ya Gaza imesema wiki kwenye taarifa kuwa, uchunguzi wa miili uliofunuliwa umeonyesha kuwa maumbo yalibadilika sana kwa sababu ya wizi wa viungo muhimu kutoka kwa maiti.
Aidha, imeongeza kuwa jeshi la Israeli limekuwa likikabidhi miili bila majina, huku likakataa kutaja kutoka mahali ambapo miili hii ilipatikana, inasema ofisi ya mawasiliano ya serikali ya Gaza imesema
Mbali na hayo, imeongeza kuwa jeshi la Israeli lilirudia kitendo kama hicho wakati wa vita vinavyoendelea Gaza na pia lilifukua miili kutoka makaburi.
Aidha, taarifa hiyo imekosoa kile ilichosema " kimya cha mashirika ya kimataifa yanayohudumu kule Gaza, pamoja na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, kuhusiana na uhalifu mbaya kama huo na uvamizi wa (Israeli)."
Mamlaka ya Israel bado haijatoa tamko juu ya mashtaka hayo.
Makaburi ya halaiki
Mapema wiki hii, mamlaka ya Israeli iliachilia miili ya Wapalestina kadhaa waliouawa na jeshi la Israeli waliowekwa kizuizini wakati wa operesheni yake ya ardhini.
Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza ilipokea miili hiyo kupitia mpaka wa Kerem Shalom kusini mwa Gaza, kulingana na mwandishi wa Anadolu katika eneo hilo.
Wizara ya masuala ya Kidini ya Gaza ilikuwa inasimamia mazishi yao katika makaburi ya halaiki, alisema mwandishi huyo.
"Umoja wa Mataifa ulitujulisha mapema juu ya kuwasili kwa mashuhadaa kadhaa huko Gaza, inakadiriwa kuwa karibu miili 80," marwan Al Hams, mkurugenzi wa Hospitali ya Mohammed Yousef El Najar katika jiji la Rafah, aliiambia Anadolu.
"Miili ilifika ndani ya kontena, zingine zikiwa zimebaki, wakati zingine zilikuwa vipande vipande, na zingine zilikuwa zimeoza," aliongeza.