Moshi ukifuka kufuatia mfululizo wa mashambulizi ya anga ya Israel kwenye eneo la Dahiyeh huko Beirut, Lebanon, Novemba 23, 2024. / Picha: AA

Jumamosi, Novemba 23, 2024

0851 GMT - Mashambulizi ya anga ya Israel yamesababisha vifo vya takriban watu 11 na kujeruhi makumi ya watu katikati mwa Beirut, wakati wanadiplomasia walipokuwa wakihangaika kutayarisha mpango wa kusitisha mapigano.

Ulinzi wa raia wa Lebanon ulisema idadi ya waliofariki ni ya muda kwani wahudumu wa dharura wangali wakichimba vifusi wakitafuta manusura.

Mashambulizi hayo yalikuwa ya nne katika mji mkuu wa Lebanon katika kipindi cha chini ya wiki moja.

0840 GMT - Wavuvi wawili waliuawa katika shambulio la anga la Israeli kwenye ufuo wa kusini mwa Lebanon

Wavuvi wawili waliuawa katika shambulio la anga la Israel kusini mwa Lebanon, kulingana na shirika rasmi la habari la nchi hiyo.

Shirika la Habari la Kitaifa la Lebanon liliripoti kwamba shambulio hilo lililenga moja kwa moja kundi la wavuvi kwenye ufuo wa wilaya ya Tiro, na kuua angalau wawili.

0807 GMT - Jeshi la Israeli laamuru kuhamishwa katika vitongoji vya kusini mwa Beirut

Jeshi la Israel liliamuru kuhamishwa kwa wakaazi kutoka kwa majengo katika maeneo ya Hadath na Choueifat Al-Amrousieh katika vitongoji vya kusini mwa Beirut.

Katika taarifa yake, msemaji wa jeshi la Israel Avichay Adraee aliwaonya wakaazi akisema: "Lazima muondoe majengo haya na yale yaliyo karibu nao mara moja na kusogea umbali wa angalau mita 500."

Adraee alidai maeneo yaliyolengwa yana "vifaa na maslahi ya Hezbollah", kuashiria shambulio zaidi wa Israel katika eneo hilo.

0716 GMT - Indonesia inakaribisha vibali vya kukamatwa kwa ICC kwa waziri mkuu wa Israel, mkuu wa zamani wa ulinzi

Indonesia imekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wa kutoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant.

Katika taarifa yake Jumamosi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia ilieleza kuunga mkono juhudi za kimataifa za kuhakikisha uwajibikaji kwa uhalifu unaofanywa na Israel dhidi ya Palestina, ikiwa ni pamoja na hatua zinazotekelezwa kupitia ICC.

"Utoaji wa hati za kukamatwa na ICC kwa Benjamin Netanyahu na Yoav Gallant unawakilisha hatua muhimu ya kufikia haki kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita huko Palestina," ilisema taarifa hiyo.

339 GMT - Makombora matano ya Israeli yanashambulia jengo la makazi katikati mwa Beirut

Makombora matano ya Israel yalishambulia jengo la makazi katikati ya mji wa Beirut siku ya Jumamosi, vyombo vya habari vya serikali ya Lebanon viliripoti.

"Beirut, mji mkuu, iliamshwa na mauaji ya kutisha, wakati jeshi la anga la adui wa Israel liliharibu kabisa jengo la makazi la ghorofa nane na makombora matano kwenye Mtaa wa Al-Mamoun katika eneo la Basta," Shirika la Habari la Taifa liliripoti.

Waandishi wa habari wa AFP walisikia angalau milipuko mitatu mikubwa katika mji mkuu.

TRT World