Serikali ya Malaysia imeonya kuhusu kifungo cha jela hadi miaka mitatu kwa mtu yeyote anayenunua au kuuza saa za Swatch zenye mandhari ya LGBTQ.
Mamlaka ilisema agizo hilo lilikusudiwa "kuzuia kuenea kwa mambo ambayo yanaathiri au yanaweza kuathiri maadili" katika taifa hilo lenye waislamu wengi ambapo uhusiano wa jinsia moja umepigwa marufuku.
Saa za rangi ya upinde wa mvua zilizotengenezwa na mtengenezaji wa saa wa Uswidi zimepigwa marufuku nchini kwa "kukuza, kuunga mkono, na kuhalalisha harakati za LGBTQ+."
Mnamo Mei, polisi walifanya uvamizi kwenye maduka ya Swatch kote nchini na kukamata vitu 172.
Zilkuwa sehemu ya bidhaa zilizotengenezwa kuunga mkono LGBTQ+, Swatch walisema.
Agizo la hivi punde linasema kwamba "uchapishaji, uagizaji, uzalishaji, toleo, mauzo, usambazaji au umiliki" wa saa za Swatch zenye "LGBTQ+" "ambayo ina uwezekano wa kuathiri maadili hairuhusiwi kote Malaysia".
Inakuja chini ya Sheria ya Vyombo vya Uchapishaji, Wizara ya mambo ya ndani iliongeza.