Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kuidhinisha Azimio ambalo linataka pande zote za Gaza kuruhusu "utoaji salama na usiokuwa na vizuizi wa misaada ya kibinadamu kwa wingi."
Azimio hilo lililopitishwa pia linataka kuundwa kwa "masharti ya kukomesha uhasama endelevu" lakini halikutoa maoni juu ya usikitishwaji wa mapigano mara moja.
Urusi na Marekani, ambazo zote zingeweza kupiga kura ya kukataa hatua hiyo kama wanachama wa kudumu wa Baraza, hazikushiriki, ikimaanisha lilipitishwa kwa kura 13 za kuunga mkono.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema baada ya kura hiyo kwamba mashambulizi ya Israel ndio "tatizo halisi la kusababisha vikwazo vikubwa" kusaidia usafirishaji, kwani alirudia wito wake wa kusitisha mapigano ya kibinadamu mara moja.
Mzozo wa kidiplomasia katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Mjini Manhattan uliosababisha kura kuahirishwa mara kadhaa wiki hii umejiri licha ya hali ya Gaza kuzorota na kuongezeka kwa idadi ya vifo.
Milki ya Kiarabu ilifadhili Azimio hilo, ambalo lilirekebishwa katika maeneo kadhaa muhimu ili kupata maelewano.
Balozi wa UAE katika Umoja wa Mataifa Lana Zaki Nusseibeh alisema "inajibu kwa hatua kufuatia hali mbaya ya kibinadamu."
"Tunajua hili sio Azimio kamili. Hatutachoka kamwe kutaka kusitishwa kwa mapigano kwa ajili ya hali ya kibinadamu," alisema.
Pia linapendekeza uteuzi wa mratibu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kusimamia na kuthibitisha misaada ya nchi za nje kwa Gaza.
Azimio la awali lilikuwa limesema kwamba utaratibu wa misaada wa kuharakisha utoaji wa misaada utakuwa "pekee" chini ya udhibiti wa Umoja wa Mataifa.
Sasa linasema utasimamiwa kwa kushauriana na" vyama vyote husika " ikimaanisha Israeli itahifadhi usimamizi wa uendeshaji wa utoaji wa misaada.
Wanachama wa Baraza la Usalama lenye washiriki 15 walikuwa wakivutana kwa siku nyingi ili kupata msingi wa pamoja juu ya azimio hilo, kwani ukosoaji uliongezeka juu ya ukosefu wa hatua ya baraza hilo tangu kuanza kwa vita.
Israel, ikiungwa mkono na mshirika wake Marekani, imepinga neno "kusitisha mapigano," na Washington imetumia kura yake ya turufu mara mbili kuzuia maazimio yanayoungwa mkono na idadi kubwa ya wanachama wengine.
Mnamo Jumatano, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema hakutakuwa na makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza hadi "kuondolewa" kwa Hamas.
Mzozo juu ya azimio hilo ulikuja wakati mfumo wa ufuatiliani wa njaa wa Umoja wa Mataifa ulipoonya "kila mtu katika Gaza iliyoharibiwa na vita anatarajiwa kukabiliwa na viwango vya juu vya ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula katika wiki sita zijazo."