Baraza la seneti lamthibitisha  mwanamke wa kwanza mwislamu kuwa jaji mahakama kuu

Baraza la seneti lamthibitisha  mwanamke wa kwanza mwislamu kuwa jaji mahakama kuu

Nusrat Jahan Choudhury sasa amethibitishwa kuwa Jaji wa mahakama kuu huko mashariki ya New York.
Nusrat Choudhury appears before the U.S. Senate Judiciary Committee in Washington / Photo: Reuters

Baraza la Seneti la Marekani lilithibitisha kwa mujibu wa vyama siku ya Alhamisi Nusrat Jahan Choudhury kuwa mwanamke wa kwanza Mwislamu na Mmarekani wa kwanza wa Bangladesh kuhudumu kama jaji wa shirikisho.

Seneti iliidhinisha kwa kiasi kidogo uteuzi wa Choudhury katika kura 50-49 huku Seneta wa Kidemokrasia Joe Manchin akiungana na Warepublican wote kupiga kura katika upinzani.

Sasa atakuwa Jaji wa wilaya huko Marekani katika wilaya ya Mashariki ya New York.

Choudhury hapo awali aliwahi kuwa mkurugenzi wa kisheria katika kikundi cha umoja wa haki za kiraia cha Marekani (ACLU) baada ya kuwa naibu mkurugenzi wa mpango wa haki ya kijamii wa ACLU.

Wasifu mfupi uliowekwa kwenye tovuti ya ACLU unasema ameongoza juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi wa aina yoyote.

Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Columbia, Chuo Kikuu cha Princeton, na Shule ya Sheria ya Yale.

Kiongozi wa Wengi katika Seneti Chuck Schumer alipongeza uthibitisho wa Choudhury, akisema anajivunia kumpendekeza kwa Rais Joe Biden.

"Anaweka historia kama Mmarekani wa kwanza wa Bangladesh na mwanamke wa kwanza mwislamu mmarekani kuhudumu kama jaji wa mahakama kuu," aliandika kwenye Twitter.

ACLU pia ilituma pongezi zake kupitia Twitter, ikisema "Nusrat ni wakili wa haki za kiraia na uthibitisho wake utakuwa muhimu kwa mfumo wa sheria wa taifa letu."

Manchin, Mwana democrat pekee aliyepinga uteuzi wake, alisema katika taarifa iliyotolewa Jumatano kwamba "baadhi ya taarifa za awali za Bi. Choudhury zinatilia shaka uwezo wake wa kutokuwa na upendeleo kuelekea kazi ya utekelezaji wetu wa sheria shupavu."

"Kama mfuasi mkuu wa wanaume na wanawake wanao simamia usalama nchini, nilipinga uteuzi wa Bi Choudhury," alisema.

TRT Afrika na mashirika ya habari