Erdogan alisema kuwa Ankara imetekeleza sera ya kuingia nchini bila pasipoti kwa wasafiri wa Kiromania. / Picha: AA

Uturuki na Romania wameweka lengo la dola bilioni 15 katika biashara ya pande mbili, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.

"Thamani ya biashara ya pande mbili kati ya |Uturuki na Romania ilizidi dola bilioni 10 kwa miaka miwili mfululizo," Erdogan alisema katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Jumanne na Waziri Mkuu wa Romania Marcel Ciolacu aliyekuwa akitembelea ikulu ya rais huko Ankara.

"Lengo letu ni kufikia dola bilioni 15," aliongeza.

Erdogan pia alisema kwamba Ankara imeweka sera ya kutokuwa na haja ya pasipoti kwa wasafiri wa Romania.

"Tumeweka kanuni ambayo itawawezesha raia wa Romania kusafiri kunigia nchi yetu kwa kadi yao ya kitambulisho," Erdogan aliongeza.

Mwezi uliopita, Makamu wa Rais wa Uturuki Cevdet Yilmaz alisema kwamba uwekezaji wa moja kwa moja wa Uturuki nchini Romania umefikia dola bilioni 7.5, akiongeza kuwa Romania ni moja ya nchi kumi bora miongoni mwa nchi wanachama wa EU ambako kampuni za Uturuki zinawekeza, na katika sekta ya ujenzi, ni nchi inayoshika nafasi ya kwanza barani Ulaya.

TRT World