Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akizungumza wakati wa Mkutano wa Mukhtars wa Istanbul uliofanyika Istanbul, Oktoba 19, 2024. / Picha: AA

Rais wa Uturuki amethibitisha uungaji mkono mkubwa wa nchi hiyo kwa Palestina huku Israel ikiendelea kufanya mashambulizi mabaya katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Gaza.

Kama "adui wa wakandamizaji na mlinzi wa wanaokandamizwa," Uturuki inasimama bega kwa bega na Palestina katika "mapambano yake ya uhuru na utu dhidi ya mtandao wa mauaji ya halaiki", Recep Tayyip Erdogan alisema wakati wa mkutano huko Istanbul uliofanyika na viongozi wa eneo hilo siku ya Jumamosi.

"Marekani, Ulaya na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimekuwa vichekesho tu mikononi mwa muuaji mkatili anayejulikana kama Netanyahu," Erdogan alisema, akimzungumzia waziri mkuu wa Israel.

Akiashiria idadi ya vifo vya watoto katika mashambulizi yanayoendelea ya Israel dhidi ya Gaza, alisema, "watoto 20,000 wamekufa. Hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza kusema, 'hii ni aibu'."

"Maelfu ya wanawake wamekufa, na mashirika ya kutetea haki za wanawake hayajatamka neno lolote," aliongeza.

"Waandishi wa habari 175 wamekufa, na vyombo vya habari vya kimataifa havijali hata kidogo," Erdogan alisema.

"Jukumu la mauaji ya watu wasio na hatia 50,000 bila shaka linatokana na vikosi vya Israel vinavyoikalia kwa mabavu kinyume cha sheria," rais wa Uturuki alisisitiza, akiongeza kuwa wale "wanaotoa msaada usio na masharti kwa serikali ya Israel na kutuma silaha na risasi pia wanashiriki waziwazi katika mauaji haya".

Erdogan alionyesha heshima kwa viongozi na wanachama wa muqawama wa Palestina, "ambayo imekuwa hadithi sio tu kupitia mapambano yao bali pia kwa mauaji yao ya shahidi, na kwa mashujaa wote ambao wameinywesha ardhi ya Gaza kwa damu yao iliyobarikiwa."

"Namtakia rehema za Mungu Yahya Sinwar, kiongozi wa Hamas ambaye aliuawa shahidi hivi majuzi," aliongeza.

TRT World