Katika siku ya tatu ya mkutano, majadiliano katika ngazi tofauti yamefanyika, ikiwemo Baraza la Utawala.
Ukifikia takriban watazamaji bilioni 3.5 na wajumbe wake 230 kutoka nchi 65. Umoja wa Utangazaji wa Pasifiki na Asia (ABU) ni jumuia kubwa zaidi duniani ya utangazaji.
Mkutano Mkuu wa 61 wa ABU umehodhiwa na TRT. Katika siku ya tatu ya mkutano, chini ya uenyekiti wa Mkurugenzi Mkuu wa TRT Mehmet Zahid Sobacı, mikutano ilifanyika katika ngazi ya urais na Baraza la Utawala.
Katika mikutano hiyo, mpango kazi wa miaka mitatu ulijadiliwa.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mkurugenzi Mkuu wa TRT Mehmet Zahid Sobacı, ambae pia amehudumu kama rais wa ABU tangu 2023, amesisitiza umuhimu wa mikutano hiyo, akisema, “Bado tunapambana kutatua changamoto za vyombo vya habari, kujadiliana mawazo, na bila shaka, kufanya maamuzi muhimu ambayo yataathiri mustakbali wa ABU.”
Siku ya tatu ya Mkutano Mkuu pia ilihusisha Mkutano wa Kamati ya Ufundi, Mkutano wa Kundi la Michezo, na Utangazaji wa Jukwaa Lote. Katika mikutano ya ushirikiano wa pamoja na Indonesia na Mongolia, fursa za ushirikiano kati ya Uturuki na nchi hizo ulifanyiwa tathmini.
Mkutano kuendelea kwa Tamasha la 13 la Nyimbo
Katika siku ya tatu ya Mkutano Mkuu, Tamasha la Nyimbo lilifanyika.
Shughuli hiyo, ilijumuisha wasanii kutoka nchi 11 wakionyesha utajiri wa tamaduni za eneo la Asia na Pasifiki.
Ilifanyika Jumapili, Oktoba 20, saa mbili usiku katika ukumbi wa kimataifa wa Istanbul Lütfi Kırdar na tukio hilo litarushwa mubashara kupitia TRT Music.
Jumanne, Oktoba 22, ufunguzi rasmi wa mkutano wa 61 wa ABU utaanza kwa hotuba ya Mkuu wa Mawasiliano Fahrettin Altun, Mkurugenzi Mkuu na rais wa ABU Mehmet Zahid Sobacı, na Katibu Mkuu wa ABU Ahmet Nadeem.
Sherehe hizo zitaangazia athari za akili mnembe na teknolojia za kidijitali katika utangazaji duniani na changamoto mpya zinazojitokeza.
Jioni hiyo hiyo, Sherehe ya Tuzo za ABU itafanyika, ambapo washindi wa tuzo katika vipengele 15 vya televisheni, redio na dijitali, watapata tuzo zao zilizoratibiwa na Umoja huo wa Utangazaji wa Asia na Pasifiki.