Rais Recep Tayyip Erdogan alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev na kumpongeza kwa ushindi wake katika uchaguzi wa Rais. / Picha: Jalada la AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa Azerbaijani Ilham Aliyev na kumpongeza kwa ushindi wake katika Uchaguzi wa Rais.

Wakati wa mkutano huo, Erdogan alieleza matumaini yake siku ya Jumatano kwamba kuchaguliwa tena kwa Aliyev kama Rais kungekuwa na manufaa kwa Azerbaijan.

Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev amepokea zaidi ya asilimia 93 ya kura katika uchaguzi wa mapema wa rais, kulingana na matokeo ya awali.

Aliyev alijipatia asilimia 93.9, mwakilishi wa Kundi la Ushauri la Oracle lenye makao yake nchini Marekani, George Brinbaum, alisema katika taarifa ya habari katika mji mkuu Baku baada ya upigaji kura kumalizika saa 1 jioni kwa saa za nchi hiyo siku ya Jumatano (1500GMT).

Mpinzani wa karibu wa Aliyev, mgombea huru Zahid Oruj, alipata asilimia 1.8 tu, kulingana na matokeo hayo.

Takriban watu milioni 6.5 walikuwa na sifa ya kupiga kura, ikiwa ni pamoja na wale walio nje ya nchi, katika uchaguzi huo.

Uchaguzi wa mwisho wa rais, ambao unafanyika kila baada ya miaka saba nchini Azerbaijan, ulikuwa tarehe 11 Aprili, 2018. Amri iliyosainiwa na Aliyev mwishoni mwa mwaka jana ilisogeza mbele uchaguzi kutoka tarehe yao ya awali ya Oktoba 2025.

TRT World