Waziri wa Mambo ya Nje Mevlut Cavusoglu | Picha: AA

Muundo wa usalama wa Ulaya "ni wazi haufanyi kazi tena" katika viwango vinavyotarajiwa, waziri huyo anaongeza.

Akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Usalama la Istanbul siku ya Jumanne, Mevlut Cavusoglu alisema, "Ni wazi kwamba muundo wa usalama wa Ulaya haufanyi kazi katika kiwango ambacho tungependa (Uturuki).

Akibainisha kwamba si "busara au jambo la kimantiki kufikiria muundo mpya wa usalama" wakati vita vya Ukraine vikiendelea, Cavusoglu aliongeza zaidi, "mchango wa Uturuki, ambayo iko mstari wa mbele kama mshirika mkuu na wa kimkakati katika usalama wa nchi za magharibi, ni muhimu sana.

Mkutano wa Usalama wa Istanbul, ambao unafanyika Mei 2-3, utashughulikia vitisho vya usalama vya kikanda na kimataifa, na suluhisho, kulingana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Jukwaa hilo la kimataifa linatarajiwa kujumuisha takriban wazungumzaji 70 wa ndani na nje ya nchi, wakiwemo wanasiasa, watunga sera, wasomi, wataalamu, waandishi wa habari na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.

Akikumbusha kwamba asilimia 60 ya migogoro na mivutano ya kimataifa inatokea karibu na nchi ya Uturuki, Cavusoglu alisema usalama "ni dhana inayovuka tofauti kama vile usalama unaotumia nguvu zaidi au usalama wa unaokuja kwa ushawishi, na inahitaji kushughulikiwa kwa kina."

Njia tatu za kuimarisha usalama

Akiorodhesha njia tatu za kuhakikisha usalama katika mazingira ya sasa, waziri wa mambo ya nje wa Uturuki alisema mojawapo ni "kuifanya nchi husika kuwa imara na kujenga ustahimilivu katika mambo yake yote."

"Wakati majeshi yaliyojizatiti na jamii imara vinapokutana pamoja na kuwa na usimamizi mzuri, mafanikio huja yenyewe. Ndiyo maana sisi (Uturuki) tumeiweka sekta ya ulinzi kama mojawapo ya maeneo ya kipaumbele," aliongeza.

Akisema kwamba Uturuki daima inasimama na washirika wake ingawa baadhi ya washirika wameikatisha tamaa Uturuki, Cavusoglu alisema.

"Najisikia aibu sana kuona kuna haja ya kutoleana wito baina ya Washirika kwamba wasiwekeane vikwazo," alisema.

Cavusoglu alibainisha zaidi kuwa njia ya pili ya kuhakikisha usalama ni “kuiweka ajenda ya usalama kama kipengele muhimu kwa wadau wote."

"Ugaidi ni moja ya vitisho viwili vikuu kwa NATO, na Washirika wote lazima waungane katika vita dhidi ya janga hili," alisema, akisisitiza kwamba Uturuki ni "nchi ambayo inapambana kwa dhati na ugaidi kuanzia ngazi za chini kabisa."

Akitoa wito kwa washirika wake wote kwamba Uturuki ndiye "mshirika pekee wa kweli katika mapambano dhidi ya ugaidi," Cavusoglu pia alisisitiza kwamba Uturuki haiwezi kamwe kuwa mshirika wa kundi la kigaidi linaloua raia na askari wa nchi mshirika.

Akitoa wito kwa washirika wake wote kwamba Uturuki ndiye "mshirika pekee wa kweli katika mapambano dhidi ya ugaidi," Cavusoglu pia alisisitiza kwamba Uturuki haiwezi kamwe kuwa mshirika wa kundi la kigaidi linaloua raia na askari wa nchi mshirika.

Waziri huyo aliendelea kusema kwamba "kuangalia usalama kwa mtazamo mpana na kutafuta suluhisho zenye ufanisi" ni njia ya tatu ya kuhakikisha usalama.

Akisema kwamba "Uturuki ni taifa lenye hekima, ukarimu, uadilifu, na ushawishi ambalo hutumia nyezo zote muhimu kwa pamoja," Cavusoglu aliahidi "kudumisha msimamo wetu kama mhusika mkuu wa usalama wa kimataifa, kwa msimamo wetu wa kibinadamu na sera yetu ya kigeni inayoongazia sana biashara ili kutatua mahitaji ya wakati husika."

TRT Afrika na mashirika ya habari