Balozi wa Uturuki Mehmet Pacaci amechaguliwa kuwa mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimtaifa ya Kiislamu (OIC), atakayeshughulikia chuki dhidi ya Uislamu.
Mehmet Pacaci alipata uteuzi huo wakati wa kikao cha 15 cha OIC, kilichofanyika mjni Banjul kati ya Mei 4 na 5, na kutangazwa siku ya Jumapili na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.
"Tuna matumaini makubwa kuwa Balozi Pacaci atatekeleza majukumu yake kwa mafanikio."
"Tungependa kuikumbusha jumuiya ya kimataifa juu ya haja ya kuonesha msimamo na dhamira ya pamoja katika kupambana na chuki dhidi ya Uislamu," wizara hiyo ilisema katika taarifa yake ya maandishi.
Nafasi za awali za Pacaci
Akiwa ni mwanadiplomasia na profesa wa chuo kikuu, Mehmet Pacac amehudumu kama balozi wa Uturuki nchini Pakistan tangu 2022.
Pia ni Mwakilishi Binafsi wa Mwenyekiti wa OSCE katika Ofisi ya Kupambana na Ubaguzi dhidi ya Waislamu.
Hapo awali, Pacaci aliwahu kuhudumu kama Balozi wa Uturuki mjini Vatican, kati ya 2014 hadi 2019.
Amewahi pia kuwa Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kigeni katika Urais wa Masuala ya Kidini mjini Ankara na Mwambata wa Urais wa Masuala ya Kidini katika Ubalozi wa Uturuki mjini Washington.