Uchunguzi wa mahakama na utawala umezinduliwa kuchunguza tukio hilo, wizara ya ulinzi ya Uturuki  inasema. / Picha: AA

Takriban wafanyikazi watano wamekufa katika mlipuko kwenye kiwanda cha roketi na vilipuzi kilichopo katika mji mkuu wa Uturuki Ankara, kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa ya nchi hiyo.

"Mlipuko ulitokea katika Kiwanda cha Roketi na Vilipuzi cha MKE katika wilaya ya Elmadag ya Ankara. Kutokana na mlipuko huo, wafanyakazi wetu watano wameuawa shahidi," wizara ilisema katika taarifa yake Jumamosi.

Imeongeza kuwa uchunguzi wa mahakama na utawala umezinduliwa ili kuangalia tukio hilo.

Kituo ambacho mlipuko huo ulitokea mapema asubuhi kinamilikiwa na Shirika la Viwanda la Mitambo na Kemikali la Uturuki (MKE).

TRT World