Mama Emine Erdogan amezuru Baraza kuu la wanawake na Baraza Kuu la Uzazi na Utoto huko Abu Dhabi, Falme za Kiarabu. / Picha: AA

Mama wa Taifa Uturuki Emine Erdogan ametembelea Umoja Mkuu wa Wanawake huko Abu Dhabi, katika mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Mama Emine ambaye ameungana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika ziara yake UAE kama sehemu ya ziara ya Ghuba, siku ya jumatano, pia alitembelea warsha za jadi za kazi za mikono, ambapo aliweza kukutana na wanawake wanaofanya kazi mbalimbali za ufundi.

Alishiriki katika Baraza Kuu la uzazi na utoto na kutembelea Msikiti Mkuu wa Sheikh Zayed na Louvre Abu Dhabi, jumba la makumbusho la sanaa lililoko kwenye Kisiwa cha Saadiyat.

Mama Emine alisifu juhudi za umoja huo katika kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya wanawake wa UAE kupitia programu mbalimbali za elimu, na kuwapa ujuzi wa kitaaluma.

Aliongeza kuwa sera zinazotengenezwa na umoja huo kuhakikisha ushirikishwaji wa kina mama hasa katika maendeleo endelevu zina manufaa makubwa.

AA