Serikali ya Kenya inasema inalenga kuboresha viwanda vya serikali vya maziwa na kufungua vingine vipya/ Picha kutoka Ikulu ya Kenya 

Serikali ya kenya inalenga kuboresha viwanda vya serikali vya maziwa, 'Kenya Cooperative Creameries' na kuweka viwanda vingine vipya vya maziwa kote nchini ili maziwa mengi zaidi yaweze kuchakatwa.

Kwa mara ya kwanza nchini Kenya, maziwa ya ngamia yatafanywa kuwa maziwa ya unga.

"Hii ni hatua muhimu kwa wakulima wetu wa ngamia, ambao wameachwa nyuma kwa muda mrefu sana," makamu wa rais Rigathi Gachagua amesema katika uzinduzi wa kiwanda cha serikali katika kaunti ya Nyeri.

Kenya in takriban ngamia milioni nne na laki sita hasa katika eneo la kaskazini mwa nchi.

Kiwanda hili kinalenga pia kuwainua wafugaji wadogo wadogo wa ng'ombe wa maziwa ambao watapata mahali pa kuboresha maziwa yao.

Kiwanda hiki kinalenga pia kuwainua wafugaji wadogo wadogo wa ng'ombe/ Picha kutoka Ikulu Kenya

Rais William Ruto alisema serikali imeweka mipango itakayowezesha uzalishaji kuongezeka kutoka lita bilioni 5.2 hadi lita bilioni 10 kwa mwaka.

Serikali inasema kuwa maziwa ni mojawapo ya vyanzo vikuu vya mapato nchini Kenya, vinavyozalisha angalau Sh200 bilioni kwa mwaka.

“Tunataka kunufaika zaidi kutoka kwa maziwa yaliyoongezwa thamani. Wakulima wetu hawastawi kwa sababu wamekuwa wakiuza maziwa mabichi,” alisema.

Alisema nchi ina vifaa vya kutosha kutengeneza unga na maziwa ya muda mrefu ili kuhakikisha maziwa ya ziada hayapotei.

TRT Afrika