Hii ni wiki ya tatu ya maandamano ya kupinga ushuru. / Picha: Reuters

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Kenya waliwarushia vitoa machozi waandamanaji jijini Nairobi siku ya Jumanne huku maandamano yakizuka katika miji mengine mikubwa nchini humo yakimtaka Rais William Ruto ajiuzulu.

Hii imefuatia makabiliano makali ya wiki mbili katika maandamano ya kupinga mswada wa fedha.

Maandamano hayana viongozi wengi ni vijana/ picha Reuters 

Moshi wa mabomu ya kutoa machozi ulitanda katikati ya jiji la Nairobi baada ya waandamanaji kuwasha moto kwenye barabara ya Waiyaki, barabara kuu inayopita katikati mwa mji mkuu, na kuwarushia mawe polisi katika wilaya ya kati ya biashara.

Nje ya mji mkuu, mamia ya waandamanaji waliandamana Mombasa, mji wa pili kwa ukubwa nchini Kenya, kwenye pwani ya Bahari ya Hindi.

Rais William Ruto, anakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa urais wake wa takriban miaka miwili/ picha Reuters 

Walibeba makuti, wakiimba "Ruto lazima aende!"

Ruto, anayekabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa urais wake wa takriban miaka miwili, amenaswa kati ya matakwa ya wakopeshaji kama vile Shirika la Fedha la Kimataifa IMF kupunguza nakisi, na idadi kubwa ya watu nyumbani wanaolalamika kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.

Maandamano mengine yalifanyika Kisumu, Nakuru, Kajiado, Migori, Mlolongo na Rongo, kulingana na picha zilizotangazwa kwenye televisheni ya Kenya/ picha: Reuters

Wanachama wa vuguvugu la maandamano, ambalo halina viongozi rasmi na ambao wengi hupanga kupitia mitandao ya kijamii, wamekataa ombi la Ruto la mazungumzo, hata baada ya kuachana na mapendekezo ya nyongeza ya ushuru ambayo yalichochea maandamano.

Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNHCR) imetoa ripoti kuwa watu 39 wamekufa katika maandamano ya wiki mbili iliyopita/ Picha: AFP 

Maandamano mengine yalifanyika Kisumu, Nakuru, Kajiado, Migori, Mlolongo na Rongo, kulingana na picha zilizotangazwa kwenye televisheni ya Kenya.

Baadhi ya Wakenya wameuawa katika maandamano na makabiliano na polisi tangu Juni 18, wengi wao wakipigwa risasi na maafisa Jumanne iliyopita, wakati baadhi ya waandamanaji walipojaribu kuvamia bunge kuwazuia wabunge kupiga kura ya nyongeza ya ushuru.

Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNHCR) imetoa ripoti kuwa watu 39 wameuawa katika maandamano , polisi wakilaumiwa.

TRT Afrika