ECOWAS, Umoja wa Afrika zakashifu jaribio la kupindua serikali Niger

ECOWAS, Umoja wa Afrika zakashifu jaribio la kupindua serikali Niger

Katika taarifa ECOWAS imetaka waliopanga majaribio ya mapinduzi ya serikali wamuachilie huru rais
Mohamed Bazoum ni rais wa Niger / Picha: Others 

Mamlaka ya ECOWAS linasema imepokea habari za jaribio la mapinduzi nchini Niger "kwa mshtuko".

Katika taarifa iliyotoa ECOWAS, muungano wa nchi za Afrika magharibi imesema " ina laani vikali jaribio la kunyakua mamlaka kwa nguvu na kutoa wito kwa wapanga mapinduzi ya kijeshi kumwachilia huru rais (Mohamed Bazoum) aliyechaguliwa kidemokrasia mara moja na bila masharti."

Imetishia kuwa waliopanga njama watawajibika kwa usalama wa rais na wajumbe wa serikali na familia ya rais.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, amelaani vikali kile alichosema kilionekana kuwa jaribio la mapinduzi nchini Niger na kuwataka wanajeshi "wahaini" waliohusika kusita mara moja.

TRT Afrika