Shirikisho la Riadha la Nigeria (AFN) limemkaribisha tena mwanariadha Favour Ofili baada ya Shirikisho la Riadha Duniani kukataa ombi lake la kubadilisha uraia michezoni.
Katika taarifa siku ya Alhamisi, AFN ilithibitisha kuwa mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 23 bado yuko vizuri kuiwakilisha Nigeria, kumaliza utata wa miezi kadhaa kuhusu ushiriki wake kimataifa.
Shirikisho hilo la riadha duniani lilikataa ombi lake, likieleza wasiwasi kuwa weledi kwenye michezo. Kulingana na AFN, ombi hilo lilitathminiwa pamoja na maombi mengine 10.
Licha ya kutambua mazingira binafsi ya Ofili, ikiwemo uwakilishi wake katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, jopo liliamua kuidhinisha kubadili uraia kungesababisha utata kimataifa.
Wito wa kuungwa mkono
Akizungumzia kuhusu uamuzi huo, AFN ilitoa wito, ikitaka mwanariadha huyo aungwe mkono.
Rais wa AFN Tonobok Okowa anasema ni wakati wa kumuwekea mazingira bora Ofili ili aweze kufanya vizuri michezoni.












