Watu wanaoingia katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutoka maeneo yanayodhibitiwa na serikali walikaguliwa zaidi huku mamlaka ikijaribu kudhibiti kuenea kwa Ebola.
Hii ni baada ya mtu mmoja kuthibitishwa kuwa na maambukizi katika jiji hilo, ambalo bado liko chini ya himaya ya waasi wa M23.
Katika kituo cha ukaguzi cha Kanyarutshinya katika eneo la Nyiragongo, kaskazini mwa Goma na mojawapo ya sehemu kuu za kuingia jijini madereva na abiria walitakiwa kuacha magari, kunawa mikono, kuvaa barakoa na kupimwa joto kabla ya kuendelea na safari.
Mamlaka zilisema hatua hizo zililenga kuzuia maambukizi katika jiji hilo lenye zaidi ya watu milioni mbili, kitovu cha kimkakati cha kibiashara kinachopakana na Rwanda.
ZILIZOPENDEKEZWA















