| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Ligi ya Mabingwa Ulaya, nani kupiga hatua?
Mkondo wa pili wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya unarindima Jumanne. Kuna mechi za kutazamiwa hasa kutaka kujua nani ataibuika kidedea.
Ligi ya Mabingwa Ulaya, nani kupiga hatua?
Wachezaji wa PSG wakifanya mazoezi uwanja wa Anfield, Liverpool. / Reuters
tokea masaa 17

Liverpool itakuwa nyumbani Anfield ikijaribu kupidnua meza dhidi ya mabingwa wa sasa Paris Saint-Germain, huku Barcelona ikisafiri hadi kwa mahasimu wa Hispania Atletico Madrid.

Chochote kinaweza kutokea katika Ligi hii. Kikosi cha Arne Slot, Liverpool kilifungwa 2-0 wiki iliopita na mabingwa wa Ulaya PSG, jijini Paris. Vijana hao wa Anfield watatarajia kuwa wanaweza wakabadilisha matokeo.

Huenda ikawa mechi ya mwisho kwa Salah, Andrew Robertson na pengine Slot kuiwakilisha Liverpool katika hatua ya ngazi ya Ulaya na hili linaweza kuwapa hamasa ya kujizatiti kupata matokeo mazuri.

Barcelona nao wanakwenda katika mji mkuu wa Hispania kukipiga na mahasimu wao wa Ligi ya La Liga, Atletico Madrid.

Atletico iliwafunga 2-0 kwenye robo fainali ya mkondo wa kwanza huku wakiwa wanajiandaa kupambana na aidha Arsenal au Sporting Lisbon kwenye nusu fainali. Hiyo iwapo watafanikiwa kupata matokeo mazuri kwa jumla.

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajiwa kufanyika mjini Budapest Mei 30, 2026.

 

CHANZO:TRT Afrika Swahili