| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Ghana yamtimua Kocha Addo wiki chache kabla ya Kombe la Dunia
Kupigwa kalamu kwa Kocha Addo unakuja baada ya timu ya taifa ya mpira ya Ghana kufungwa mechi nne mfululizo katika mechi za kirafiki.
Ghana yamtimua Kocha Addo wiki chache kabla ya Kombe la Dunia
Black Stars, ambayo iko katika kundi moja na England katika Kombe la Dunia, imepoteza mechi nne za kirafiki. / / AP
tokea masaa 13

Shrikisho la Soka la Ghana limetangaza kumfukuza kazi kocha Otto Addo, saa chache baada ya kupoteza mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani, siku 72 kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia.

 “The Black Stars” walipoteza kwa mabao 2-1 katika mechi iliochezwa mjini Stuttgart, Ujerumani siku ya Jumatatu, na kuwa, na kuwa kipigo cha nne mfululizo kwa kocha Addo, ambapo pia timu yake ilipokea kichapo cha 5-1 kutoka kwa Austria, wiki iliyopita.

Hii ilikuwa kipigo cha nne mfululizo kwa timu ya Addo, ambayo ilifungwa 5-1 na Austria wiki iliyopita.

"Shirikisho limemshukuru Otto Addo kwa dhati kwa mchango wake kwa timu na linamtakia kila la heri katika mustakbali wake," ilisema Shirikisho la Soka la Ghana (GFA).

Shirikisho hilo limesema litatoa taarifa zaidi kuhusu mwelekeo mpya katika wakati muafaka.

Addo mwenye umri wa miaka 50 amekuwa kocha wa timu ya Ghana tangu Machi 2024.

Ghana ipo kwenye kundi moja na England, Croatia, na Panama katika michuano ya Kombe la Dunia itakayochezwa Amerika Kaskazini.

CHANZO:AFP