tokea masaa 2
Timu ya Real Madrid iko Ujerumani nyumbani kwa Bayern Munich —mabingwa hao mara nyingi walifungwa na Bavaria nyumbani kwao robo fainali mkondo wa kwanza 2-1. Magoli ya Bayern yalifungwa na Harry Kane na Luis Diaz huku la kufutia machozi kwa Real Madrid likiwekwa kimiani na Kylian Mbappe katika kipindi cha pili.
Lakini pia macho yote yatakuwa yakiangazia Arsenal ambao katika Ligi Kuu ya England wamekuwa wakisuasua katika siku za hivi karibuni. Arsenal inaingia katika mkondo huu wa pili wakiwa na ushindi wa 1-0 dhidi ya Sporting CP ya Ureno huko jijini Lisbon.
Mechi hiyo ya robo fainali mkondo wa pili itachezwa katika uwanja wa Emirates, jijini London.
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajiwa kufanyika mjini Budapest Mei 30, 2026.
CHANZO:TRT Afrika Swahili














